Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari ACT Wazalendo walia na tozo, kodi za mazao
HabariHabari Mchanganyiko

ACT Wazalendo walia na tozo, kodi za mazao

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema kodi na tozo za mazao zinachangia kurejesha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo na wakulima kwa ujumla. Anaripoti Rhoda Kanuti … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 18 Mei 2022, na Naibu Msemaji wa Sekta ya Kilimo na Mifugo, Suleiman Misingo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya bajeti iliyowasilishwa na Wizara ya Kilimo jana tarehe 17 Mei 2020, bungeni Dodoma.

Misango amesema tozo na kodi za mazao ndizo zinazokwambisha maendeleo ya kilimo nchini na kufanya wakulima kuwa na hali duni.

Ametaja mfano wa tozo sita zinazokatwa kwenye zao la korosho nchini kama vile:-Tozo ya Bodi ya Korosho shilingi 30, Tozo ya Halmashauri Shilingi 65, Tozo ya chuo cha Naliendele Shilingi 25, Tozo ya chama Kikuu Cha Ushirika Shilingi 30, Tozo ya chama Cha Msingi Cha Ushirika Shilingi 25, Tozo ya kuchangia Elimu Halmashauri Shilingi 30 na Tozo ya usafirishaji korosho Toka ghala la AMCOS hadi ghala la Chama Kikuu Cha Ushirika (inategemea na umbali).

Aidha, kuhusu suala la stakabadhi ghalani ambapo amesema mfumo huo unatakiwa kuboreshwa kutokana na kasoro zinazowaumiza wakulima.

“Mfumo huu umekuwa ukiacha maumivu kwa wakulima wetu badala ya kuwa msaada—tofauti na ilivyotarajiwa. Changamoto ya mfumo huu ni kuwa hakuna ushirikishwa wa moja kwa moja kuhusu kuamua bei ya mazao ya wakulima.

“Pili, ucheleweshwaji wa malipo kwa wakulima (wakulima wanakopwa) jambo ambalo wakulima wengi hawawezi kumudu, hatimaye wanauza kwa watu wa kati (Kangomba) kwa bei ya chini zaidi (wananyonywa)” amesema Misango.

ACT- Wazalendo imesisitiza serikali kujenga miundombinu mizuri vijijini na mashambani kwa ajili ya kuboresha kilimo ikiwa pamoja na kuimarisha mfumo wa kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua. Pia upatikanaji wa mbolea na matumizi ya zana za kisasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!