Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo wahofia usalama wa Zitto
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo wahofia usalama wa Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeeleza kuwepo kwa hofu ya kudhuriwa Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 10 Februari 2019 Kudra Garula, Mratibu wa Ulinzi na Usalama wa Ngome ya vijana wa chama hicho amedai kuwa zipo taarifa za kuwindwa kwa kiongozi huyo.

Amesema, tahadhari ya ‘watu wasiojulikana’ waliokuwa wakimwinda Tundu Lissu ilitolewa lakini uovu wa kushambuliwa kwake ulitekelezwa.

Garula amesema, Zitto ameanza kutishwa na kufuatiliwa na watu wenye nia ovu ambao kwa bahati mzuri wamewajua.

“Hivi karibuni kiongozi wetu akiwa kwenye shughuli za kibunge huko Dodoma, alifuatwa
na kijana ambaye alijitambulisha kwake kama Ofisa usalama wa Taifa na kumwambia kuwa,
dawa yake ni kumuua,” amesema na kuongeza;

“Kamati yetu ya Ulinzi na Usalama baada kupata taarifa hizo ikaanzisha opereshe ya kumsaka na kumtambua kijana huyo.

“Baadaye kumtambua kuwa ni kijana wa UVCCM jambo ambalo lilitushangaza,” amesema.

Ameleeza kuwa, baada ya tukio hilo Zitto alimuandikia barua Job Ndugai, Spika wa Bunge kumjulisha na kwamba, baadaye spika alimwita muongo.

“Sisi kama ngome tunaamini kuwa upo mpango wa kumteka na kumdhuru Ndugu Zitto Kabwe,” amesema na kuongeza;

“Tunazo taarifa za kuwa wapo watu wanamfuatilia kiongozi wetu kwa lengo la kumuua.”

Amedai, Jumatano tarehe 6/2/2019 usiku walishtukiwa baadhi ya watu waliokuwa
wakimufuatilia Zitto lengo likiwa ni kumdhuru lakini wabunge wenzake walimuhamisha na kumpeleka sehemu salama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!