Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo ‘wachomoa betri’
Habari za SiasaTangulizi

ACT-Wazalendo ‘wachomoa betri’

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amekiondoa chama hicho kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 24 Novemba, 2019. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi ndogo ya chama hicho, leo tarehe 8 Novemba, 2019, Magomeni jijini Dar es Salaam, kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema, hawatakubali Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiendelee kufurahia uchaguzi huo.

“Hii nchi ni yetu sote, wote tumeapa kulinda Katiba, haiwezekani sheria iwe kwa ajili ya vyama vya upinzani halafu CCM waendelee kuvunja, haitawezekana,” amesema Zitto na kuongeza;

“Safari hii hatujiondoi kama ambavyo CCM imezoea, hapana. Tunaendelea na vikao na tumekuwa tunawasiliana na vyama vingine ili kuamua hatua ya kuchukua.”

Zitto amesema, chama hicho kimeondolewa wagombea wake na ambapo wameachiwa asilimia nne tu (4%).

“Wanasema CCM wanapenda sana, kwanini waweke mpira kwapani. Tumeachiwa asilimia nne, maana yake watawala wametuondoa ili wabaki wenyewe wapite bila kupingwa,” amesema.

Amesema, wananchi wengi wamekuwa wakiwaonya kwamba uchaguzi hautokuwa wa haki, lakini waliendelea kuhamasisha watu kujiandikisha kwa kuwa, ni haki yao kupiga kura.

Zitto amesema, licha ya miaka minne ya changamoto na wananchi wengi kuonya kwamba uchaguzi hautakuwa wa haki, ACT-Wazalendo kiliamua kushiriki katika uchaguzi.

Amesema, zaidi ya wanachama 173,000 wa ACT-Wazalendo walijitokeza kuchukua fomu na kuzirejesha, lakini kwenye watu wao wote, jumla ya wagombea wetu 166,000 wameondolewa.

https://www.youtube.com/watch?v=osWT2VjZEIU

“Tunduru jumla ya vijiji zaidi ya 70, tumeachiwa wagombea wawili tu, Tandahimba tulikuwa na wagombea 73 vijiji lakini mpaka saa 6 walibakizwa watano tu. Mji mdogo Kilwa Kivinje wagombea wote wameondolewa, Kibamba na Kigamboni Dar es Salaam wagombea wetu wote wameondolewa.

“Jimbo la Ilala, mitaa yote tumebakiziwa wagombea wawili tu na sababu zinaoteolewa hazina uzito. Tanga katika mkoa mzima tumebakiziwa asilima 18, Kigoma Mjini mitaa yote 68 tulisimamisha wagombea, mpaka leo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya Kigoma, tumebakiziwa saba tu,” amesema Zitto.

Amesema, wasimamizi wamekuwa wakitoa sababu zisizo na mashiko huku wengine wakitumia jina la chama hicho kuchukua fomu.

“Kuna baadhi ya maeneo, watendaji wamefanya mambo ya kihuni, mtaa wa Feri Kigamboni, kuna mgombea amepandikizwa, ambapo sisi hatumjui. Kachukua fomu kwa niaba ya ACT-Wazalendo, halafu katika tarehe ya kadi ya chama, ameandika yeye amepata kadi ya chama tarehe 13 Machi 2000, ACT imesajiliwa mwaka 2014 lakini yeye alikuwa na kadi ya ACT-Wazalendo miaka 14 kabla ya ACT kusajiliwa.”

Amesema, katika mazingira kama hayo, ACT-Wazalendo imeondolewa kwenye ushindani kwa madai, watawala hawataki kushindana.

“Hii maana yake watawala hawataki kushindana, licha ya kwamba watawala wametumia miaka minne kukandamiza shughuli za kisiasa za vyama, wamefanya siasa peke yao,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!