April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo waanza kuwashughulikia CCM

Mbarara Maharagande, Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalumu ya Chama cha ACT-Wazalendo

Spread the love

MAJIMBO yanayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa yapo kwenye meza ya viongozi na makada wa Chama cha ACT-Wazalendo huku kila mmoja akieleza anataka lipi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Makada na wanachama wa chama hicho, sasa wanataa majimbo wanayotaka kugombea katika Uchaguzi Mkuu unaotaajiwa kufanyika Oktoba 2020 huku wakiapa kutumia njia mbalimbali kuhakikisha wanayatwaa.

Mbarara Maharagande, Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalumu ya Chama cha ACT-Wazalendo, amesema anakwenda kumng’oa Bonnah Kamoli katika Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Maharagande ametangaza nia hiyo leo tarehe 6 Mei 2020. Ameomba ridhaa ya chama chake kumteua kupeperusha bendera yake, kwenye uchaguzi kupitia jimbo hilo.

“Mimi Mbarala Abdallah Maharagande, napenda kuchukua fursa hii kutia nia na kutangaza rasmi kuwa, natarajia kuomba ridhaa ya chama changu cha ACT Wazalendo kugombea nafasi ya Ubunge wa Segerea, Dar es Salaam katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2020.”

Maharagande amejitokeza baada ya Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, kuwataka wanachama wa chama hicho wanaohitaji kugombea katika nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo, kutangaza nia.

“Nachukua nafasi hii kuunga mkono wito wa chama uliotolewa na katibu mkuu wa chama, kuwataka wanachama wote wenye lengo la kugombea nafasi ya udiwani, ubunge na au urais kupitia ACT Wazalendo, kutangaza nia,” ameeleza Maharagande.

Haruna Muyango, mwanachama wa chama hicho, ametangaza kumng’oa Peter Serukamba ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM).

Muyango amesema, anakwenda kuchukua jimbo hilo lililotelekezwa na Serukamba ambaye amekaa kwenye jimbo hilo kwa miaka mitano sasa bila kuwakwamua wananchi wake.

Suphian Juma, aliyekuwa Ofisa Habari wa chama hicho ameapa kutumia mbinu mbalimbali ili kutwaa Jimbo la Singida Magharibi. Kwa sasa Elibariki Kingu ndio mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM.

“Mimi Suphian Juma, natangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Singida Magharibi kupitia Chama cha ACT wazalendo, Singida Magharibi nitawatanguliza ninyi na Taifa langu mbele daima. Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie,” amesema Suphian.

error: Content is protected !!