Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Tunakuja kwa kishindo
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Tunakuja kwa kishindo

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado
Spread the love

 

WAKATI vyama vya siasa vya upinzani vikianza kutangaza ratiba ya kuanza mikutano ya hadhara, Chama cha ACT-Wazalendo kimesema Kamati yake Kuu, itakutana hivi karibuni kupanga mikakati ya utekelezaji wa suala hilo ili kije kwa kishindo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 7 Januari 2023 na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, akizungumza na MwanaHALISI Online, kuhusu ruksa iliyotolewa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

“Maamuzi ya kufunguliwa au kuondoa zuio la mikutano ya hadhara tumeyapokea na kwa chama chochote makini kwa uamuzi huo mnahitaji mkae chini kwenye vikao muweze kutoka na ratiba na utekelezaji ili mtoke kwa kishindo,” amesema Ado na kuongeza:

“Kamati Kuu itaitishwa katika siku chache zijazo na itatoa kalenda ya operesheni kuhusu mikutano ya hadhara.”

Kauli hiyo ya ACT-Wazalendo inakuja baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kutangaza ratiba yake ya kufanya mikutano ya hadhara ambapo leo Jumamosi Mwenyekiti wake Prof. Ibrahim Lipumba, anatarajiwa kuzindua mkutano huo katika Viwanja vya Manzese Bakhresa, wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Nacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuzindua mikutano ya hadhara kitaifa tarehe 21 Januari 2023, ingawa hakijataja eneo ambalo zoezi hilo litafanyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!