January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo kuzindua ‘Azimio la Tabora’

Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Sabini Richard (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Said Sanani Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Spread the love

JUNI 13 mwaka huu, Chama cha ACT-Wazalendo kinatarajia kuzindua Azimio la Tabora mara baada ya kumaliza kikao chake cha Halmashauri Kuu kitakachofanyika mkoani humo. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumzia kikao hicho kitakachofanyia kwenye Ukumbi wa Community Center, Katibu Mawasiliano na Uenezi Taifa, Sabini Richard amesema, lengo la kikao hicho ni kukamilisha hatua za kuliendea azimio hilo.

Na kwamba, kikao hicho kitapitisha kalenda ya Uchaguzi Mkuu pamoja na mikakati mbalimbali inayohusu chama hicho katika kuelekea uchaguzi ujao baadaye mwaka huu.

“Kichama, wiki hii tumeiita ni wiki ya Azimio la Tabora kwa kuwa, Mkutano Mkuu huu ni wa kihistoria na  utafanyika huko,  ukiwa na ajenda kuu tatu muhimu sana,” amesema Richard.

Amezitaja ajenda hizo kuwa ni pamoja na kupokea na kujadili taarifa ya ziara katika mikoa 10 iliyofanyika Aprili mwaka huu, pili; kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa oparesheni ya Majimaji.

Tatu ni kupokea, kujadili na kupitisha Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha litakaloongoza utekelezaji wa siasa ya ujamaa wa kidemokrasia ya Chama cha ACT.

Amesema, “tumeamua kufanyia mkutano huu mkuu Tabora  tukienzi historia ya mkoa huo katika ukombozi wa Taifa letu ambapo matukio makubwa ya ukombozi yalifanyika.”

Aidha amesema, baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Juni 14 chama kitaanza ziara katika mikoa sita, ambayo ni Geita, Kagera, Kasulu, Kigoma mjini, Katavi, Rukwa na Mbeya.

Richard ametoa wito kwa wakazi wote wa Tabora na mikoa mingine, kuhudhuria mikutano yote itakayofanyika ili kukiunga mkono chama hicho.

error: Content is protected !!