Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo kuanza na mambo 10 Ikulu
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo kuanza na mambo 10 Ikulu

Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetaja hatua 10 itakazochukua kuimarisha sekta binafsi na uwekezaji, endapo kitafanikiwa kushika dola. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).  

Hatua hizo zimetajwa leo tarehe 22 Septemba 2020, Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkoani Tabora.

Zitto amesema, serikali itakayoundwa na ACT-Wazalendo na vyama washirika, itapitia upya mifumo yote ya kodi ili kuwe na kodi rafiki kwa wafanyabiashara, pamoja na kuondoa mfumo unaolazimisha wafanyabishara kulipa kodi kabla ya kuanza biashara.

“Itapitia mifumo yote ya kodi na kuhakisha kunakuwa na kodi rafiki kwa wananchi ili kuhakisha biashara zinakua na kuimarika, siyo kuwa na mfumo wa kodi ambao utapelekea kufunga au kuua biashara. Itaondoa mfumo unaomlazimisha mfanyabiashara kulipa kodi kabla hajaanza kufanya biashara,” amesema Zitto.

Hatua ya tatu ni, kuwapa wananchi Uhuru na kuondoa urasimu katika kuanzisha na kuendesha biashara yoyote ikiwa ni pamoja na Uhuru wa kununua na kuuza bidhaa zozote halali ndani na nje ya nchi bila vikwazo vyovyote.

“Hatua ya nne, itarasmisha udalali wa kiasili kwa kuutambua, kuupa leseni na masharti ya kuwezesha Haki katika Biashara ya Mazao,” amesema Zitto.

Zitto amesema, hatua ya tano ni ufufuaji na uendelezaji wa viwanda vya kuchakata pamba na kuzalisha nguo, kwa kutunga sera na sheria zitakazowezesha kupambana na biashara haramu ya nguo pamoja na kutoa msamaha wakodi kwa malighafi za viwanda vya nguo.

“Serikali yetu itatoza ushuru wa forodha kwa kiwango sifuri Kwa vifaa vyote ambavyo ni malighafi kwa viwanda vya nguo na kutoa mikopo maalumu kwa kipindi maalumu yenye riba ya kiwango cha mfumuko wa bei kwa mnyororo wa thamani wa pamba mpaka nguo,” amesema Zitto.

Hatua ya sita ni kutoa ruzuku ya kikodi kufidia gharama za uzalishaji kwa viwanda vinavyozalisha bidhaa zinazotumiwa na wananchi wengi zaidi kama vile Sukari, Mafuta ya kula na vitabu na karatasi kwa kulipia asilimia 50 ya gharama za umeme.

Zitto amesema, hatua ya saba ni kutoa ruzuku kwa kampuni za utalii ili kuimarisha sekta hiyo iliyotetereka kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19).

“Tutarekebisha sera za kodi ili kuirejesha katika hali yake ya kawaida sekta ya utalii pamoja na mnyororo wake ambayo imeathirika sana na janga la COVID 19.

“Marekebisho hayo yatahusisha kutoa ruzuku kwa kampuni za utalii na kulinda ajira za Wafanyakazi wa Sekta ya Utalii,” amesema Zitto.

Hatua ya nane ni kuweka vivutio vya kikodi ili kuwezesha sekta binafsi kujenga miundombinu wezeshi kwa mfumo wa ubia. Ili kuipa serikali nafasi ya kujielekeza kwenye kutoa huduma muhimu kwa wananchi, kuepuka kuongeza deni la taifa na kukuza sekta binafsi.

“Hatua ya tisa Itaweka vivutio vya kibajeti na kikodi kwenye miradi yote ya kilimo cha umwagiliaji na viwanda vyote vya kuongeza thamani ya mazao ya Kilimo,” amesema Zitto.

Hatua ya mwisho ni kurekebisha muundo mzima wa makato kutoka kwenye mapato ya waajiri na waajiriwa ili kuchochea matumizi kwenye uchumi.

Kwa kupunguza kodi ya mapato kwa wafanyakazi (PAYE), kima cha chini mpaka asilimia nane kutoka asilimia tisa ya sasa kwa kuanzia mapato ya Sh. 500,000 kwa mwezi na kiwango cha juu mpaka asilimia 25.

“Kurekebisha tozo ya kuongeza ujuzi kwa kuishusha mpaka asilimia 2 na italipwa na Wwaajiri wote ikiwemo Serikali na taasisi zake zote.

Kupunguza makato ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) mpaka asilimia m bili kwa ujumla wake (mwajiri asilimia 7 na mwajiriwa asili mia 5), Bima ya Afya na Fidia kwa Wafanyakazi itajumuishwa katika Mafao ya Hifadhi ya Jamii,” amesema Ziito.

Zitto amesema “Tutaimarisha sheria ya kuzuia ukwepaji wa kodi kwa makampuni ya kimataifa ili kuokoa mapato sawa na asilimia tano ya pato la Taifa ambayo yanapotea kupitia mbinu za kihasibu zinazofanywa na Multinational Corporations. Kuwezesha hili Serikali itaingia mikataba ya kimataifa inayosadia mataifa kuzuia ukwepaji wa kodi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!