Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Kangi Lugola anafanya kazi kwa kulipuka
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Kangi Lugola anafanya kazi kwa kulipuka

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo wamesisitiza kuwa Kiongozi wao, Zitto Kabwe hatatii agizo lililotolewa na Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani, kwani hana mamlaka hiyo na amekuwa akifanya kazi zake kwa kulipuka. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na vyombo vya Habari leo tarehe 1 Agosti, mwaka huu, Ado Shaibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho ameweka wazi kuwa kiongozi huyo hatotii amri hiyo kutokana na kuwa haipo kisheria.

“Nilisema wakati wa uteuzi wake kuwa hatuna matumaini sana na kuteuliwa kwake kwa sababu ya hulka yake ya kufanya kazi kwa kulipuka,” amesema Ado.

Amesema kuwa utabili wake wa kuwa Lugola hawezi kuleta matumaini kwa taifa umetimia kutokana na hatua yake.

Shaibu ameeleza kuwa jopo la wanasheria wa chama wamejiridhisha kuwa wito huo sio halali na kwamba Zitto hawezi kutii amri hiyo.

Shaibu amesema msimamo huo ni heshima kwa chama hicho kwa sababu wito huo hajaitwa kwa heshima.

Amesema kuwa Zitto alikwenda Kilwa kwa ajili ya kumuunga mkono Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Seleman Bungara ‘Bwege’ kwenye utetezi wa wananchi wa maeneo hayo ambao ni wahanga wa deni ya mauzo ya nje ya zao la korosho dhidi ya serekali.

Amesema kuwa kiongozi kama Zitto hana mipaka ya kuwatetea wananchi kutokana na kuwa ni mbunge na kwamba wabunge wapo kwa ajili ya jimbo la taifa zima.

Ameeleza kuwa Zitto ataendelea na kampeni za kuwanadi wagombea udiwani wa chama chake kwenye uchaguzi mdogo utakaofanywa Tarehe 12 Agosti mwaka huu kwenye kata 77 na jimbo moja na Buyungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!