Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msajili aikamia ACT- Wazalendo, atishia kuifuta
Habari za SiasaTangulizi

Msajili aikamia ACT- Wazalendo, atishia kuifuta

Benard Membe (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe pamoja na Maalim Seif
Spread the love

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, inakusudia kukipa adhabu Chama cha siasa cha upinzani ACT-Wazalendo, kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa barua ya ofisi hiyo iliyolewa tarehe 14 Julai 2020 na Sisty Nyahoza, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, ACT-Wazalendo kilionywa mara kadhaa kuhusu ukiukwaji huo, lakini haikuchukua hatua.

“Kutokana na ukweli kwamba, tangu mwaka 2018 ACT-Wazalendo mmefanya vitendo kadhaa vya kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Msajili wa Vyama vya Siasa amekuwa akiwaasa muache kufanya hivyo, lakini hamzingatii ushauri wake.”

“Msajili wa Vyama vya Siasa anakusudia kuwapa adhabu Chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa, ili iwe fundisho kwenu na kwa Vyama vya Siasa vingine kuwa, ni muhimu kuheshimu Sheria za nchi ikiwamo Sheria ya Vyama vya Siasa katika shughuli za kisiasa na vyama vya siasa, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo inaeleza zaidi kwamba, adhabu hiyo itawakumbusha ACT-Wazalendo kwamba, Sheria ya Vyama vya Siasa inafanya kazi muda wote hata wakati wa uchaguzi

“Na kwamba, uchaguzi isiwe kigezo cha kukiuka sheria za nchi na kwamba, wakati wa uchaguzi ndiyo Vyama vya Siasa vinapaswa kuheshimu zaidi Sheria za nchi, ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu. Hivyo, mtapewa adhabu husika hivi karibuni,” inaelesa barua hiyo

MwanaHALISI Online limemtafuta leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo kuhusu barua hiyo ambapo amesema atafutwe baadaye.

Miongoni mwa makosa ambayo Chama cha ACT-Wazalendo kinadaiwa kufanya ni, kitendo cha Zitto Kabwe, kiongozi wake, kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB), kuomba isitishe kuipa mikopo Tanzania.

“Aidha, tarehe 22 Januari, 2020 Mheshimiwa Zitto Kabwe aliandika barua Benki ya  Dunia kuiomba isitishe kuipa mikopo Tanzania nchi ambayo yeye ni raia wake.”

“Mkopo huo ni kwa ajili ya kuimarisha huduma ya elimu kwa Watanzania wote ikiwamo watoto na ndugu wa wananchama wa ACT-Wazalendo,” inaeleza barua hiyo.

Ofisi ya Msajili imedai kwamba, hatua hiyo ya Zitto ilikiuka Ibara ya 29(5) na 30(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, na kifungu cha 6A(1)(2) na (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, kinachohitaji chama cha siasa kuanzishwa na kuendeshwa kwa kuzingatia misingi ya Katiba na uzalendo.

“Kuhusu uvunjifu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ambao umekuwa ukifanywa na chama chenu kupitia Kiongozi Mkuu, mara zote tulizowaandikia barua mmeshindwa kuthibitisha kuwa, hamjakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa,” inaeleza barua hiyo.

Barua ya ofisi hiyo inadai kwamba, mojawapo ya ushahidi ACT-Wazalendo kimekiuka sheria ni Zitto kutoa lugha za uongo, dhihaka na uchochezi.

Kwa mujibu wa barua hiyo, tarehe 21 Aprili, 2020, Zitto anadaiwa kutoa waraka wenye maneno ya dhihaka, uongo na uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiongea kuhusu suala Ia maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

“Kauli yake ilikuwa inakusudia kumchonganisha  Rais na wananchi. Vilevile, ilikuwa inaichonganisha nchi yetu na mataifa rafiki, kwani alieleza tuhuma ambazo hazikuwa na ushahidi wowote na zilionekana dhahiri ni maneno ya uongo,” inaeleza barua hiyo.

Vilevile, ACT-Wazalendo kinadaiwa kuvunja sheria kupitia Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wake, ambapo anadaiwa kutoa lugha zenye uchochezi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Suala lililoelezwa katika barua yenye kumbukumbu namba HA. 322/362/20/10 ya tarehe 13 Desemba 2019, linahusu video iliyokuwa katika mitandao ya kijamii, ikionyesha Mheshimiwa Seif Sharif Hamad akiwahutubia wanachama wa ACT- Wazalendo, akiwataka kubeba silaha za jadi (Panga, Shoka, Jembe, n.k.) na kuzitumia kulinda ofisi za chama chenu,” inaeleza barua hiyo.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kupitia barua hiyo, imesema chama hicho hadi sasa kimeshindwa kuthibitisha kwamba makosa hayo hayajakiuka sheria ya Vyama vya Siasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!