Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Bunge lithibitishe kama siyo dhaifu
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Bunge lithibitishe kama siyo dhaifu

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, kimelitaka Bunge la Jamhuri kuthibitisha uimara wake katika kuisimamia serikali.Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Chama kimeeleza kwamba, Bunge linapaswa kuhakikisha kuwa, kila aliyeguswa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad anachukuliwa hatua.

Kauli hiyo imetolewa na Soud Salimu, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 30 Aprili 2019 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu Ripoti ya CAG ya Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Salimu amesema, badala ya mhimili huo kumshambulia na kutekeleza azimio lake la kutofanya kazi na Prof. Assad, ni vyema likafainyia kazi hoja zake ili lithibitishie umma kwamba, sio dhaifu kama alivyoeleza mkaguzi huo.

Amesema, hatua ya Bunge kuwasimamisha wabunge kusimamia mikutano kadhaa ya Bunge kwa kuunga mkono kauli ya Prof. Assad kwamba Bunge ni dhaifu, haitalifanya bunge hilo kuwa imara.

“Bunge lijidhirishe uimara wake katika kuisimamia serikali na kuchukuliwa hatua wahusika, ichukuliwe kwa mtazamo chanya kuliko tunachokiona sasa CAG anashambuliwa,” amesema Salimu na kuongeza;

“Spika anamshambulia mbunge aliyeichambua ripoti ya CAG, tunajiuliza uimara wa bunge hili na unaadhihirishwa na nini? Kwa kufukuza wabunge au kutofanya kazi na jicho lake ambalo ni CAG.”

Aidha, Salimu amesema ACT-Wazalendo mkoa wa Dar es Salaam walifanya uchambuzi wa ripoti ya CAG na kubaini kwamba halmashauri za jiji hilo kuna maeneo kumetokea ubadhirifu.

“Ripoti imeonesha jiji na halmashauri za Dar es Salaam zimepata hati yenye kuridhisha lakini yapo maeneo kadhaa yanahitaji kutupiwa macho kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia kwamba kumetokea ubadhirifu mkubwa,” amesema Salimu.

Salimu amesema: “Tunasihi wabunge wote bila kujali vyama kutekeleza wajibu wao kuisimamia serikali.Serikali iache kumdhibitio CAG Akupitia bunge kupitia udhaifu wa spika, mamlaka ya uteuzi wa halmashauri hasa zilizofanya malipo bila mamlaka husika wakurugenzi wake wachukuliwe hatua, madiwani wafanye kazi zao ipasavyo kusimamia serikali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!