November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo: 2020 tunachukua Z’bar

Spread the love

HARAKATI za kutambulisha na kuimarisha Chama cha ACT-Wazalendo visiwani Zanzibar zinashika kasi ambapo sasa kinadai kitashinda nafasi ya urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Anaripoti Jabir Idrisa, Zanzibar … (endelea).

Salim Biman, aliyekuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF akziungumza na waandishi wa habari tarehe 19 Machi 2019 amesema, ushindi utarejea.

Amesema, nguvu iliyokuwepo CUF kabla ya kuondoka kwa Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho ndio ile ile ya ACT-Wazalendo ambayo itawawezesha kushinda uchaguzi huo.

Akizungumza baada ya upandishaji bendera kwenye Makao Makuu ya Ofisi ya ACT-Wazalendo iliyopo Vuga, Unguja Biman amesema, muda mchache ujao Wazanzibari wengi watajitokeza na kujiunga na chama hicho ili kuinua nguvu ile ile kuelekea katika ushindi.

Biman amewataka wale ambao hawajaungana na Maalim Seif kufanya uhamuzi huo kwa kuwa, safari ni ile ile ya kuikomboa Zanzibar.

Amesisitiza kuwa, Uchaguzi Mkuu ujao utakuwa wenye mafaniko makubwa kwa ACT-Wazalendo na umma wa Wazanzibari.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo amesema, chama hichi kitajiimarisha bara na visiwani kikiwa na lengo kuu la kuikomboa Tanzania yote.

error: Content is protected !!