March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

ACT wamruhusu Zitto kujiunga UKAWA

Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo

Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kimebariki msimamo wa kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe wa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani katika kusimamisha wagombea kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa majimbo mawili na kata 79. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maazimio ya kamati hiyo iliyoketi katika kikao cha kawaida kilichofanyika jana, Makamu Mwenyekiti wa ACT, Shaaban Mambo amesema kamati imeridhia chama kufanya mazungumzo na vyama vingine vya upinzani ili kuachiana baadhi ya maeneo ya kimkakati ili kuhakikisha upinzani unaibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo.

“Chama kitashiriki kwenye uchaguzi huu wa marudio, kabla ya kufikia uamuzi huu chama kilifanya jitihada kupigania mazingira ya uchaguzi huru na wa haki kwa kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi barua kuhusu vitendo vya ukiukwaji sa misingi ya kidemokrasia kwenye chaguzi zilizopita za marudio. Ni imani ya Act kuaa vyama vingine vya upinzani vitaipokea rai hii ili kuhakikisha upinzani unashinda uchaguzi,” amesema.

Wakati Act ikitangaza rasmi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani katika kusimamisha wagombea kwenye uchaguzi huo, chama cha CUF upande unaomuunga mkono Mwenyekiti wake anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umetangaza kusimamisha wagombea katika kata zote na majimbo mawili yanayorudiwa uchaguzi.

Naibu Katibu Mkuu CUF, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi huo huku akiwataka wanachama wa CUF kujitokeza kuchukua fomu za kugomea nafasi hizo.

error: Content is protected !!