July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT kupeleka Azimio la Arusha mikoani

Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Anna Mghwira (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Anna Mghwira (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Spread the love

CHAMA cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) kinatarajia kulitangaza Azimio la Arusha kwa umma. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Ziara ya kulitangaza azimio hilo itafanyika katika mikoa ya; Njombe, Iringa, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Mara.

Hatua hiyo inakuja baada ya maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika 31 Machi, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofsi za ACT, jijini Dar es Salaam Anna Mghwira – Mwenyekiti wa ACT Taifa amesema, “shughuli ya kulitangaza Azimio la Arusha itafanyika wiki ijayo baada ya sikukuu ya Pasaka.

“Ziara hiyo itawahusisha viongozi wa chama katika ngazi ya taifa kutangaza Azimio la Arusha lililohuishwa baada ya kupitishwa na vikao vya chama na kwa sasa azimio hilo lipo katika mchakato wa kuchapwa,” amesema Mghwira.

Mghwira amesema masula mengine yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni; kumuagiza Samsoni Mwigamba – Katibu Mkuu wa ACT kuanza mchakato wa kutangaza nafasi ya kuwapata wajumbe watakaoingia katika kamati ya uadilifu ya chama.

Aidha, mchakato huo pia unatakiwa ufanyike kwa ngazi zingine za chini za chama, kuhakikisha kuwa wanapata wajumbe wa kamati ya uadilifu katika ngazi husika.

Pia, Mghwira amesema “Kuhusu Katiba inayopendekezwa, tumeamua kuwa tutakaposhika madaraka ya dola baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, tutaanza na mchakato wa katiba pale ilipoishia Tume ya Jaji Joseph Warioba na sula hili tumeliweka katika Ilani yetu”.

Akijibu tuhuma za chama hicho kutumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kupunguza nguvu ya upinzani nchini hasa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mghwira amesema, “ACT haukuanzishwa kwa malengo hayo”.

“ACT ni chama ambacho wanachama wake wametoka CCM, Chadema, NCCR- Mageuzi, CUF na ambao hawakuwa na itikadi. Hatupo kwa lengo la kupambana na Chadema. Vyama vyote vya siasa ni wenzetu,” amefafanua Mghwira.

error: Content is protected !!