August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT kufumua Bajeti ya Magufuli

Spread the love

 

CHAMA cha ACT- Wazalendo kesho kitafanya kongomano la uchambuzi wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/2017,anaandika Pendo Omary.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama hicho na viongozi wengine wa ACT watachambua bajeti hiyo.

Pia wataainisha njia mbadala za kuhakikisha bajeti hiyo inalenga kuchochea ukuaji wa uchumi shirikishi na ustawi wa jamii kwa kuzingatia misingi ya usawa, uwajibikaji, demokrasia na uongozi bora.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Abdala Khamis, Ofisa Habari wa chama hicho imeeleza “Dhana kuu itakayoongoza uchambuzi ni ujenzi wa taifa lenye kujitegemea kwa kuzingatia misingi ya ujamaa wa kidemokrasia.”

Wachangiaji wengine katika kongamano hilo ni Anna Mghwira, mwenyekiti wa chama hicho; Prof. Kitila Mkumbo, mshauri wa chama na Godphrey Mwan’gonda, mchambuzi wa masuala ya uchumi.

Kongamano litafanyika ukumbi wa Millenium Towers, Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia saa 7 mchana hadi saa 11 jioni.

error: Content is protected !!