July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT: Hakuna mgombea atayepita bila kupingwa

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe

Spread the love

CHAMA cha ACT- Wazalendo kimesema hakuna mgombea atakayepita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utafanyika Oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti zoezi la uandikishaji wapiga kura limeripotiwa na vyombo vya habari kuwa na upungufu: wa uhaba wa vifaa; rushwa; baadhi ya wananchi kuandikishwa zaidi ya mara moja; vifaa kushidwa kufanya kazi na muda wa uandikishwaji kutosha.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari Venance Msemwa, Katibu Mambo ya Nje wa chama hicho amesema, “…tutasimamisha wagombea nchi nzima. Kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani. Safari hii hakuna kiongozi atakae pita bila kupigwa.”

Habibu Mchange, Katibu wa Mipango na Mikakati Taifa wa chama hicho amesema chama hicho Jumamosi wiki hii kitafanya mkutano mkubwa katika uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya operesheni mbalimbali zilizofanyika katika mikoa 22 mpaka sasa.

“Baada ya ziara na operesheni zote katika mikoa 22 nchini, sasa ACT-Wazalendo kupitia viongozi wake wa kitaifa wamefikia hatua ya kukikabidhi chama jijini Dar es Salaam kama ilivyofanyika katika mikoa mingine, kwani kila tulipopita tumekuwa tukifanya hivyo,” amesema Mchange.

Aidha, amesema katika mkutano huo watazindua ilani ya mkoa wa Dar es Salaam ambamo tayari mwaliko kwa vyama vya siasa rafiki wa chama hicho kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)metolewa.

error: Content is protected !!