January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Abwao ahoji vijana kubugudhiwa

Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Chiku Abwao (kulia) akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete. Kushoto Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Chiku Abwao (Chadema), ameitaka Serikali ieleze ni kwanini imekuwa ikiwasumbua vijana wanaokijishughulisha kujitafutia ajira. Anaadika Dany Tibason … (endelea).

Abwao alitoa kauli hiyo leo bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza, akihoji kwanini vijana hao hususani waendesha bodaboda wanasumbuliwa.

“Imekuwa ni kawaida ya serikali kuwahangaisha vijana ambao wanajitafutia riziki kwa kujiajiri wakati ikijua haiwezi kuwapatia vijana hao ajira. Je, ni kwanini wamekuwa wakisumbuliwa badala ya kuwatengea maeneo ambayo ni rafiki?

“Tumeshuhudia vijana wengi wakiangaishwa na viongozi wa halmashauri mbalimbali, ni kwanini sasa serikali isiwaboreshee maeneo ambayo ni rafiki ili kuepukana na usumbufu wanaoupata? Amehoji.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul (Chadema) katika swali lake la nyongeza alitaka kujua ni wakurugenzi wangapi wa halmashauri ambao wamechukuliwa hatua baada ya kushindwa kutenga asilimia 10 kwa ajili ya akina mama na vijana.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (Chadema), alitaka kujua serikali imetoa huduma gani kwa vijana wa Wilaya ya Kwimba ili kuwezesha kujiajiri wenyewe na kutaka kujua ni vikundi gani vimenufaika na mpango huo.

Akijibu maswali ya nyongeza, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, amesema serikali imewatuma wataalam kufuatilia ili kubaini ni halmashauri ngapi ambazo zimeweza kutenga asilimia kumi kwa ajili ya akina mama na watoto.

Naye Naibu Waziri wa Fedha, Adamu Malima, akijibu swali la msingi kwa niaba ya Waziri wa Kazi na Ajira, amesema huduma ambazo hutolewa na serikali kwa vijana wa Kwimba ni pamoja na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali na ujuzi wa uendeshaji wa mashine za kufyatua matofari.

Amesema huduma nyingine ni utoaji wa mikopo nyenye masharti nafuu kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana.

error: Content is protected !!