August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Aboud Jumbe afariki Dunia

Spread the love

ABOUD Jumbe Mwinyi, aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu, anaandika Hamisi Mguta.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, amefariki kutokana na maradhi yaliyokua yakimsumbua kwa muda mrefu hadi kufariki kwake.

Jumbe, aliwahi kuwa rais wa Zanzibar mwaka 1972-1984 na aliwahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.

error: Content is protected !!