Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Abiria, wahudumu waliookolewa wakiwa hai ajali ya ndege Bukoba hawa hapa
Habari Mchanganyiko

Abiria, wahudumu waliookolewa wakiwa hai ajali ya ndege Bukoba hawa hapa

Baadhi ya abiria waliokolewa katika ajali ya ndege ya Precision
Spread the love

MAJINA ya abiria 22 na wahudumu wawili waliookolewa wakiwa hai kwenye ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea leo asubuhi Jumapili katika Ziwa Victoria wilayani Bukoba mkoani Kagera, yametajwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Manusura wa ajali hiyo waliokimbizwa katika Hospitali ya mkoa Kagera, ni moja ya abiria 43 wa ndege hiyo iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kueleke Bukoba – Kagera.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 6 Novemba, 2022 na Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, waliookolewa wakiwa hai ni Ragi Samwel Inyoma mkazi wa Dar es Salaam, Rausath Hassan (26) mkazi wa Bukoba, Anna  Mitabalo (40) mkazi wa Karagwe na Dk. Felix Otieno (37) mkazi wa Bunda.

Wengine ni Dk. Shamiru Ismail (34) mkazi wa Bukoba, Protas Mussa (38) mkazi wa wa Ngara, Amos Skoth (38) mkazi wa Mwanza, Grace Rugambwa (67) mkazi wa Nyakanyasi Bukoba, Amina Abdallah Karwandira (62) mkazi wa Bukoba na Reviba Theonest Rutinda   (29) ambaye ni Mhandisi wa Kiwanda cga Sukari Kagera.

Amewataja wengine kuwa ni Emili Victor Mwesiga (1.3) mkazi wa Kagera, Jesca Julius  Titus (27) muuguzi mkazi wa Dar es Salaam, Zanglin (30) Mhandisi raia wa China,  Richard Komba (42) – Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chai Kagera, Emmanuel Amani (28) mkazi wa Mwanza, Nikson Jackson Kawiche (35) Mkaguzi kutoka MDH Dar es Salaam na Saleh Omary (46) mkazi wa Kipawa Karakata Dar es Salaam.

Wengine ni Edwin Bitegeko (33) mfanyakazi qa CRDB Dar es Salaam, Eva Dickson Mcharo (38) mfanyakazi wa TAKUKURU Sengerema Mwanza, Josephine Joseph Mwakisambwa  (34) mkazi wa Dar es Salaam, Theodora Stanslays Mpesha (46) mkazi aa Dar es salaam na Joseph Laurence Mbago (57) mfanyakazi wa BOT mkazi wa Dar es Salaam.

Aidha, wahudumu ndege hiyo waliookolewa wakiaa hai ni Brenda Selvuli Temba (23) mkazi wa Dar es Salaam na Lydia Ibrahim  Ramadhan (25) mkazi wa Dar es Salaam.

Amesema wanaume waliookolewa jumla ni 16, wanawake tisa na mtoto mmoja wa kiume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!