August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Abiria wa Treni kuendelea na safari leo

Spread the love

 

ABILIA 775 wa treni waliokwama Kilosa mkoani Morogoro baada ya stesheni ya Gulwe kukumbwa na mafuriko wataendelea na safari yao leo kwa usafiri wa treni ya Deluxe wakianzania Dodoma saa 2 usiku, Anaandika Pendo Omary.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa uhusiano wa Kampuni ya reli Tanzania (TRL) kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja Kungu Kadogosa abiria hao wataanza kusafiri leo baada ya mafuriko kupungua.

“Wakati taarifa hii inatolewa na Uongozi wa TRL treni iliokwama Kilosa, iko njiani kurejea Morogoro ambapo mabasi yapatayo 12 yatawasafirisha hadi Dodoma ambapo watasafiri na Deluxe kuelekea Tabora, Kigoma na Mwanza,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Hadi jana asubuhi treni 2 za abiria zilikuwa zimekwama katika stesheni za Dodoma. Treni ya Deluxe iliyokuwa inaelekea Dar es Salaam na Kidete mkoani Morogoro ilikuwa inaelekea bara.

Taarifa hiyo ilisema kuwa tayari abiria 219 wa treni ya Dodoma walipatiwa usafiri mbadala wa mabasi kuja Dar es Salaam lakini hawa wa Kidete ilitarajiwa mafuriko Gulwe yangepungua na kuiwezesha treni kupita salama.

Hata hivyo kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Kadogosa ni kwamba mafuriko yalikuwa yanaongekeza.

Aidha, Katika taarifa hiyo, uongozi wa TRL umeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria na jamaa zao waliokuwa wakiwasubiri kuwapokea katika vituo mbali mbali vya treni nchini.

 

error: Content is protected !!