July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Abiria fastjet Mwanza wafura

Spread the love

 

ZAIDI ya abiria 80 waliokuwa wanatarajiwa kusafiri na ndege ya FastJet ya saa 6:00 jana mchana kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam, walilalamika baada ya safari yao kuahirishwa, anaandika Moses Mseti.

Malalamiko hayo yalitokea saa 9:00 mchana katika uwanja huo wa ndege uliopo kilimita 10 kutoka katikati ya Jiji la Mwanza.

Abiria hao ambao wengine walikata tiketi kwa ajili ya kuondoka asubuhi saa ya saa tatu jana lakini muda ulipofika, waliambiwa waondoke wachache kwa madai hakuna ndege ya kuwatosha wote.

Hata abiria waliotakiwa kusafiri saa sita mchana, safari zao ilikatishwa na kulazimika kuondoka na ndege ya saa sita usiku kitendo ambacho kiliibua vurugu hizo.

FastJet ambao kwa sasa wana ndege mbili kutoka nne za awali, waliwaeleza wateja wao kuwa, wamefikia hatua hiyo baada ya uongozi kudai kuna upungufu wa ndege.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambae hakutaka jina lake kuandikwa gazeti ameuambia Mtandao huugazeti kwamba, abiria hao wamefikia hatua hiyo baada ya safari zao kuahirishwa.

Ezekiel Manyiga, Mwakilishi wa FastJet Mkoa wa Mwanza alipotafutwa na mtandao huu kuzungumzia suala hilo, alidai yeye si msemaji wa kampuni.

“Sikia mimi sio msemaji wa kampuni, nakuomba tafuta msemaji, atakueleza kama ni tatizo la ufundi ama kitu gani, ukiniuliza mimi sina cha kuzungumza,” alisema Manyiga.

Esta  Madale, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza alisema, suala hilo sio la kiufundi na kwamba, lingekuwa la kiufundi angelitolea ufafanuzi.

error: Content is protected !!