March 15, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Gwajima aibuka upya

Askofu Josephat Gwajima

 

ASKOFU Josephat Gwajima, kiongozi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima nchini Tanzania, ameibuka kanisani kwake katika mkesha wa mwaka mpya na kuwaeleza wafuasi wake kuwa bado anapinga vitendo vya utekaji nchini mwake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Gwajima alitoa mahubiri kwa mara ya mwisho atika kanisa hilo lililopo Ubungo jijini Dar Es Salaam, Juni 2025, kabla ya kanisa hilo kufungiwa na kuzingirwa na polisi. Kanisa hilo lilifunguliwa mwishoni mwa Novemba mwaka jana.

“…Unajua magumu yaliyokupata wewe, yalikupata kwa sababu mimi nilikataa utekaji. Mpaka leo nakataa vilele…Mungu hataki, sheria yan chi haitaki, dini nayo haitaki… nan chi nayo haitaki. Hayo yako vilevile,” alisema Gwajima akishangiliwa na wafuasi wake.

Aidha, Askofu huyo amesema kuwa anaamini Tanzania itavuka mapito yake kwa kishindo.

Gwajima ambaye alikuwa mbunge wa chama tawala nchini Tanzania alijitokeza katikati ya mwaka 2025 kuwa mpaza sauti dhidi ya matukio ya utekaji ya watu hususan walioonekana kuwa wakosoaji wa serikali.

Serikali imekuwa ikijitenga na matukio hayo ya utekaji lakini ingali inanyooshewa kidole cha lawama.

Aliyekuwa mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ana historia ya matukio na kauli zenye utata, alijitokeza kama mkosoaji wa matukio ya utekaji na watu kupotea, ambayo yamekuwepo nchini Tanzania kwa kipindi cha muda sasa hata baadhi ya watu waliotekwa kuuawa.

Ukosoaji huo, ndio umeonekana kumuingiza kwenye patashika na viongozi wakuu wa chama chake.

About The Author

error: Content is protected !!