Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 9/11: Nani aliyemuua Osama?
Habari za Siasa

9/11: Nani aliyemuua Osama?

Spread the love

TAIFA la Marekani ambalo ni kubwa na lenye nguvu leo linaadhimisha miaka 17 ya shambulio la kigaidi na lisiloweza kusahaulika kwa miaka mingi ijayo. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Shambulio hilo lilifanyika tarehe 11 Septemba 2001 ambapo sasa utambulisho wake ni 9/11. Wachambuzi mbalimbali walielezea mazingira ya tukio hilo kwa namna walivyoweza.

Osama bin Laden ndio mshukiwa mkuu wa shambulio hilo, ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa Kundi la Al Qaeda. Baada ya tukio hilo nchini Marekani chini ya utawala wa George Bush, Osama alisikika akikana kuhusika.

Hata hivyo Marekani ilisisitiza kuwa ndiye muhusika na safari ya kumsaka ilihitimishwa tarehe 2 Mei, 2011 katika Mji wa Abbottabad, Pakistan ambapo taarifa za kuuawa kwakwe zilitolewa chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Barrack Obama katika oparesheni iliyopewa jina la Neptune Spear.

Kifo cha Osama kiliacha maswali mengi kwamba je ni kweli makomando wa Marekani ndio waliomuua? Mbona hawakumuonesha kama walivyofanya kwa Saadam Hussein wa Iraq?

Pia ni kipi kilichosababisha maiti yake isiwekwe hadharani hasa kutokana ukibwa wa tukio alilohusishwa nalo? Katika hili dunia imegawika katika makundi mawili, moja linaamini kuwa Osama alikufa kwa maradhi ya kawaida na lingine linaamini aliuawa na makomando wa Marekani.

Tujikumbushe tukio lilivyotokea

Ilikuwa ni tarehe 11 Septemba 2001 ambapo dunia ilishuhudia tukio lisilomithilika kwa wamarekani wenyewe. Ni mwaka ambao mashambulio manne ya pamoja yaliyofanywa na kundi la Kigaidi la al-Qaida katika ardhi ya Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa za maofisa, imeelezwa kwamba kikosi cha Al-Qaida waliteka nyara ndege nne kama silaha huu ya kutekeleza dhamira yao katika majengo mjini New York. Shambulio hilo lilipoteza zaidi ya watu 3,000.

Ndege ya Marekani-American Airlines Flight 11 ilitekwa na Al-Qaida na kisha kuielekezwa na kugonga mnara wa Kaskazini mwa Jengo la Biashara la Kimataifa (WTC) la mjini New York. Mnara huo uligongwa saa 8:46:30 asubuhi.

Ndege ya pili iliyokuwa na jina la United Airlines Flight 175 nayo ilikuwa mikononi mwa magaidi hao na kuelekezwa kwenye mnara wa WTC la upande wa Kusini na kugonga mnara huo saa 9:02:59 asubuhi.

Tukio la kwanza halikuonwa na watu wengi lakini la pili liishuhudiwa na wengi kwa kuwa habari za kushambuliwa jingo la kwanza zilikuwa tayari zimesambaa katika mji.

Kamera nyingi za televisheni zilikuwa tayari zimeelekezwa katika eneo la tukio. Ni wakati huo ndege ya pili iligonga mnara wa Kusini mwa jengo hilo.

Ndege ya tatu yenye jina la American Airlines Flight 77 baada ya kutekwa na magaidi, ilielekezwa kwenye jengo la Pentagon la mjini Arlington, Virginia. Ni karibu kidogo na jiji la Washington DC na kuvamia jingo hilo majira ya saa 9:37:46 asubuhi.

Na ndege ya nne ya United Airlines Flight 93 ilitekwa lakini haikufanikiwa kufika mahala ilipokusudiwa na kwamba, inaaminika magaidi walitaka kulenga jingo la Mji Mkuu wa Marekani.

Lakini haikugonga jingo lolote badala yake magaidi hao waliiangusha chini saa 10:03:11 asubuhi. Taarifa zinaeleza kuwa abiria walijaribu kuinyang’anya ndege hiyo kutoka mikononi mwa magaidi hao lakini hawakufanikiwa na mwisho ilianguka karibu na mji wa Shanksville, Pennsylvania.

Jumla ya watu waliokufa katika ndege hizo walikuwa 246 na magaidi waliokufa walikuwa 19. Minara yote miwili ya jengo la WTC iliteketea kwa moto baada ya shambulio hilo. Mnara wa Kusini (WTC 2) liliungua kwa muda wa dakika 56 kabla ya kuanguka na kuangamia kabisa.

Jengo la Kaskazini (WTC 1) liliungua kwa muda wa dakikar 102 nalo pia lilianguka. Kama jengo la WTC lilivyoanguka, sehemu na mmong’onyoko wa jengo hilo ulisababisha majengo mengine yaliyoyazunguka majengo hayo kushika moto na kuharibika. Kutokaa na uharibifu uliotokea, jengo la tatu la 7- (7 WTC), nalo likaanguka saa 5:20 jioni ya siku hiyo. Baadhi ya majengo mengine yaliharibiwa vibaya na hata kuangamia kabisa yaani.

Ndege iliyogonga Pentagon iligonga chini mwa upande wa Magharibi mwa jengo hilo kisha ikagonga mpaka katika nguzo tano zinazoshikilia jengo hilo. Shambulio hilo Pentagon liliuwa watu 125.

Watu 2,973 walikufa katika shambulio hilo, wakiwemo watu watu wa zima moto waliokuwa wakijaribu kuokoa maisha ya baadhi ya watu waliopatwa na tukio hilo.

Hili lilikuwa ndio shambulio kubwa la kwanza kwa watu ambao wasio Waamerika kushambulia nchini humo tangu mwaka 1941 wakati ambao Japani waliposhambulia kituo cha Jeshi la Maji kilichopo katika Bandari ya Pearl, Hawaii.

Dhana nyingi zilikuwa zikionekana kwamba, kuna watu ndani ya Marekani walikuwa wakijua kuwa kutatokea tukio la namna hiyo kabla na ni lini litatokea. Makala hii kwa msaada wa mtandao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!