Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko 90,025 kuanza mitihani Kidato cha Sita
Habari Mchanganyiko

90,025 kuanza mitihani Kidato cha Sita

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde
Spread the love

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde amesema, takribani wanafunzi 90,025 wanatarajiwa kufanya mtihani wa Kidato cha Sita kuanzia kesho Jumatatu tarehe 3 hadi 25 Mei 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Msonde ametoa taarifa hiyo leo Jumapili tarehe 2 Mei 2021, wakati akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam.

“Kesho tarehe 3 hadi 25 Mei 2021 kutakuwa na mitihani ya kidato cha sita pamoja na ualimu ambayo itakuwa inafanyika katika taifa letu Tanzania Bara na Zanzibar,kwenye  jumla ya vituo 804 vya shule za sekondari na 248 vya kujitegemea na vyuo vya ualimu 75,” amesema Dk. Msonde.

Dk. Msonde amesema“Kwa upande wa mtihani wa kidato cha sita 92,500 ndiyo waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka huu 2021, ambapo kati yao waliosajiliwa, watahiniwa  81,343 wa shule za sekondari na   8,682 wanafunzi wa kujitegemea.”

Katibu Mtendaji huyo wa NECTA amesema, watahiniwa 46,233 kati ya 81,343 ni wavulana huku wanawake wakiwa ni 35110.

“Tunao pia watahiniwa wenye mahitaji maalum 118 kwenye mtihani huu ,  kati yao 95 wenye uono hafifu  na 23 wasioona. Kati ya watahiniwa wa kujitegemea 8,682, wanaume ni 5,759 sawa na asilimia 66.33 na wanawake 2,923 sawa na asilimia 33.67,” amesema Dk.Msonde.

Kuhusu mtihani wa ualimu, Dk. Msonde amesema watahiniwa 6973 wamesajiliwa kufanya mtihani huo katika kozi mbalimbali, ambapo 2,187 katika ngazi ya Styashahada na 4,786 wa ngazi ya cheti.

“Kwa ujumla maandalizi yote ya mitihani hii yameshakamilika ikiwa pamoja kuchapwa kwa mitihani, kusafirishwa na mitihani yenyewe na vifaa vyote vya ujibuji mitihani hiyo imefikishwa ngazi ya mikoa na halamshauri,” amesema Dk. Msonde.

Aidha, Dk. Msonde amewaonya wakuu wa shule na watahaniwa kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mitihani hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!