May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

8 wapoteza maisha mechi ya Cameroon vs Comoro

Spread the love

 

Watu nane wameripotiwa kufariki na mamia kujeruhiwa katika msongamano uliotokea nje ya uwanja uliotumika katika kinyang’anyaro cha wenyeji Cameroon na Comoro waliofuzu hatua ya nane bora kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Taarifa zinaeleza kuwa mashabiki walikuwa waking’ang’ana kuingia kwa nguvu katika uwanja Paul Biya uliopo katika mji mkuu Yaounde nchini humo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la AP, Gavana wa jimbo la kati la Cameroon Naseri Paul Biya, amesema huenda kukawa na idadi zaidi ya waathiriwa.

Taarifa nyingine zinasema kuwa watoto kadhaa walikuwa wamepoteza fahamu.

Uwanja huo una uwezo wa kuwapokea watu 60,000, lakini kwa sababu ya masharti ya kuzuia maambukizi ya Covid ulipaswa kupokea asilimia 80 pekee ya watu hao.

Maofisa wa mechi walisema kwamba watu wapatao 50,000 walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya uwanja huo.

Nick Cavell, mzalishaji wa vipindi wa BBC Afrika, alikuwa katika mechi hiyo amesema kwamba ilionekana taarifa ya mkanyagano haikuwafikia umati wa watu hadi taarifa iliporipotiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Viatu vingi na vifusi vilionekana kwenye lango la kuingia uwanjani.

Aidha, Muuguzi Olinga Prudence aliliambia shirika la habari la AP kwamba baadhi ya majeruhi walikuwa katika hali mbaya.

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limesema katika taarifa yake kwamba kwa sasa linachunguza hali hiyo ili kupata taarifa zaidi kuhusu kile kilichotokea.

Mechi ya mwisho ya 16 baina ya Cameroon na Comoro ilichezwa jana usiku tarehe 24 Januari 2022, licha ya tukio hilo na ilimalizika kwa ushindi wa wenyeji Cameroon wa 2-1 dhidi ya Comoro.

error: Content is protected !!