January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MSD yaitaka Serikali kukomesha Polio

Spread the love

BOHARI ya dawa nchini kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Afya wametakiwa kuhakikisha kwamba chanjo ya polio inasambazwa katika mikoa iliyokusudiwa haraka iwezekanavyo. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya kwa vyombo vya habari na kusainiwa imesema wizara imepokea dawa miloni mmoja ambapo zimehifadhiwa katika bohari ya dawa ya taifa (MSD) na kiasi hicho kitatosheleza miezi miatu pekee.

Nsaschris Mwanjala  ni msemaji wa Wizara hiyo ameweka bayana kuwa dawa hizo zinatarajiwa kusambazwa katika mikoa 16  yenye uhaba mkubwa wa dawa za chanjo ya polio kwa watoto.

Sababu kubwa iliyotwajwa uya uhaba kwenye mikoa hiyo imetokana na  ucheleweshwaji katika taratibu za ununuzi na hivyo kupelekea kikosekana kwa chanjo hiyo kwa wakati.

Ametoa wito wa kuwataka Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) na waganga wakuu mikoa kuhakikisha kwamba chanjo hizo zinafika katika vituo vya afya na kusambazwa kwa walengwa.

Aidha wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha usambazaji usambazaji wa chanjo na vifaa husika unafanyika kwa wakati na kuzingatia usimamizi shirikishi ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

error: Content is protected !!