SERIKALI ya Kenya, imetangaza wagonjwa wapya 727 wa virusi vya corona (COVID-19) baada ya kupima sampuli 6,371 ndani ya saa 24 zilizopita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kenya imekuwa na utaratibu wa kutoa taarifa za COVID-19 kila siku na leo Jumamosi tarehe 1 Agosti 2020, Waziri wa Afya nchi humo, Mutahi Kagwe amesema, maambukizo yamefikia 21,363.
Amesema, wagonjwa 23 wamefariki dunia akiwemo mtoto wa miaka 16 hivyo kufanya idadi ya waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo kufikia 364.
Kagwe amesema, kati ya wagonjwa hao wapya, 696 ni Wakenya na 31 ni raia wa kigeni ambapo 465 ni wanaume na 262 ni wanawake.
Waziri huyo amesema, Jiji la Nairobi limeendelea kuwa na maambukizo makubwa kati ya wagonjwa hao wapya, 470 wanatoka jijini humo.
Amebainisha maeneo wanayotoka wagonjwa hao ndani ya Jiji la Nairobi kuwa ni Kiambu (64), Kajiado (25), Kirinyaga (20), Mombasa (16), Migori (15), Busia (13), Machakos (12) na Laikipia wagonjwa 11.
Waziri huyo amesema, wagonjwa 254 wamepona corona ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya waliopona kufikia 8,419.
Leave a comment