May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Orlando Pirates yaikaushia Simba

Spread the love

 

KLABU ya Orlando Pirates ya nchi Afrika Kusini, mpaka sasa haijatoa taarifa kuwa ni lini inatarajia kuingia nchini, kwa ajili ya mchezo wa robo faibali wa michuano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kwanza wa robo fainali utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 1 kamili usiku tarehe 17 Aprili 2022, huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa tarehe 24 Aprili 2022, Soweto Afrika Kusini.

Taarifa zinaeleza kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sambamba na klabu ya Simba zimewatumia taarifa timu hiyo kutaka kujua wamnawasili lini nchini tayari kwa mchezo huo, lakini uongozi wa klabu hiyo mpaka sasa haijajibu chochote juu ya ujio wao.

Usili huo unakuja kufuatia mchezo huo kuwa na uzito mkubwa, huku wakikumbuka ndugu zao Kaizer Chief msimu uliopita walipoteza kwa mabao 3-0, dhidi ya Simba kwenye hatua kama hii kwenye michuanop ya Ligi ya Mabingwa licha ya kufanikiwa kufuzu.

Orlando wanakuja nchini huku wakijua ubora wa Simba na jinsi wanavyojua kutumia vizuri dimba lao la nyumbani, licha ya upande wao kuwa na rekodi ya kuwa timu iliyopachika mabao mengi kwenye hatua ya makundi.

Katika hatua ya makundi Orlando amepachika jumla ya mabao 15, katika michezo sita waliocheza huku wakiruhusu mabao matano kwenye wavu wao.

Kwa upande wa Simba kwenye hatua ya makundi walifanikiwa kupachika mabao tisa na kuruhu saba, kwenye michezo sita waliocheza.

error: Content is protected !!