Spread the love

 

SERIKALI ya Uingereza imewawekea vikwazo mabinti wa Rais Putin wa Urusi wanaofahamika kwa majina Katerina Vladimirovna Tikhonova na Maria Vladimirovna Vorontsova ,Pamoja na binti wa Waziri wa mambo ya nje ya Urusi Sergei Lavrov anayejulikana kwajina la Yekaterina Sergeyevna Vinokurova. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa BBC … (endelea).

Katika taarifa hiyo kwenye vyombo vya Habari, ofisi ya Mambo ya Nje , Serikali ya Uingereza imesema kwamba inalenga zaidi maisha ya kifahari ya watu wa karibu wa Kremlin ,marufuku kusafiri kwa watu hao

Kwa mujibu wa serikali ya Uingereza, imesema kuwa kitendo cha vita cha Putin sasa kimehifadhiwa na vikwazo vilivyoratibiwa vya Uingereza na kimataifa katika wiki za hivi karibuni.

Hata hivyo imeongeza kuwa Urusi inaendelea kwenye mdororo mkubwa zaidi wa uchumi , tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovieti huku vikwazo vikiathiri uwezo wa Rais huyo , kwakuanzisha vita nchini Ukraine .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *