Spread the love

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2021 huku yakionesha somo la Basic Mathematics ndilo somo pekee ambalo ufaulu wake upo chini ya wastani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde yameonesha kuwa watahiniwa wamefanya vizuri katika masomo mengi ya msingi ambapo ufaulu wa masomo hayo uko juu ya wastani kati ya asilimia 55.33 na 95.58.

Aidha, watahiniwa hawakufanya vizuri katika somo moja  la Basic Mathematics, ambapo ufaulu wa somo hili upo chini ya wastani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *