Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko 6 wadakwa tuhuma za mauaji ya daktari Tarime, mfanyakazi GGML
Habari MchanganyikoTangulizi

6 wadakwa tuhuma za mauaji ya daktari Tarime, mfanyakazi GGML

Marehemu Milembe Selemani
Spread the love

HATIMAYE Jeshi la Polisi nchini limewadaka watuhumiwa watatu wa mauaji ya Dk. Isack Daniel Athumani aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kerende kilichopo Tarime Rorya mkoani Mara.

Pia limewadaka watuhumiwa wengine watatu waliodaiwa kutekeleza mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) Milembe Selemani. Mtuhumiwa wa nne katika mauaji ya mfanyakazi huyo anadaiwa kujinyonga baada ya wenzie kudakwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo 15 Mei 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime amesema uchunguzi unakamilisha ili watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani.

“Mtakumbuka kuwa Mei 3, 2023 yaliripotiwa mauaji ya Dk. Isack Daniel Athumani ambaye alikuwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Kerende kilichopo Tarime Rorya akitokea kazini.

“Tukio hilo lilifanywa na watu ambao
hawakuweza kufahamika kwa mara moja.
Jeshi la Polisi lingependa kuwajulisha kuwa watuhumiwa watatu waliofanya mauaji hayo pamoja na kukimbilia Mwanza na baadaye Dar es Salaam wamekamatwa na askari wetu waliobobea katika uchunguzi wa matukio ya
mauaji,” amesema na kuongeza

“Mtakumbuka tarehe 26 Aprili 2023 katika mtaa wa Matulole, Kata ya Buhalahala
mkoani Geita, kulitokea mauaji ya mfanyakazi mmoja wa Mgodi wa GGM kwa
jina la Milembe Selemani @ Hungwa yaliyofanywa na watu ambao hawakuweza kufahamika kwa wakati huo.

Dk. Isack Daniel Athumani enzi za uhai wake

“Kutokana na uchunguzi makini wa askari wanaochunguza matukio ya mauaji, wamefanikiwa kukamata watuhumiwa watatu na wameonyesha vielelezo walivyotumia katika mauaji hayo pamoja na baadhi ya mali za marehemu, wakati wowote watafikishwa mahakamani,” amesema.

Amefafanya kuwa mtuhumiwa wa nne, baada ya kupata taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu
wenzake na kwamba askari wamefika nyumbani kwake, aliamua kujihukumu
mwenyewe kwa kujinyonga.

Amemtaja mtuhumiwa huyo kwa majina ya Pastory Lugodisha @ Buchuchu na alijinyonga tarehe 6 Mei 2023 kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Wiayani Sengerema.

Pamoja na mambo mengine amesema Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wahalifu ambao hawataki kuachana na vitendo vya kihalifu ili kufanya kazi halali, watambue kuwa wakifanya uhalifu wowote ule, iwe mchana au usiku ni lazima watakamatwa kwa njia yeyote ile na itakuwa ni aibu kwao na kwa familia zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

error: Content is protected !!