Spread the love

 

HOMA imeanza kupanda kwa baadhi ya mawaziri, naibu mawaziri na wabunge, kutokana na kauli ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwa atafanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Miongoni mwa wanaoelezwa kuwa homa imeanza kuwapanda na kuwashuka, kuwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa sasa, Kassim Majaliwa, ambaye naye hajajua hatima yake.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya Serikali na kwa watu wa karibu na Rais Samia, Amiri Jeshi Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, anatarajia kufanya mabadiliko hayo, mwanzoni mwa Februari 2022.

Hatua hiyo, inazidisha homa kwa nafasi ya Majaliwa kuendelea ama kuenguliwa kwenye wadhifa huo, alioanza kuutumikia Novemba 20, 2015, alipoapishwa na Rais John Magufuli.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema leo Ijumaa 7 Januari 2022, kujua sura hizo mpya na maoni ya mchambuzi wa masuala ya kisiasa akizungumzia mabadiliko hayo na uchaguzi 2025 unavyoathiriwa na kifo cha aliyekuwa Rais, John Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *