MWANDISHI wa riwaya nchini Tanzania Abdulrazak Gurnah ametuzwa tuzo ya amani ya Nobel katika fasihi 2021 kutokana na kuangazia suala la ukoloni na athari zake katika utunzi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Profesa huyo wa fasihi ametangazwa mshindi leo tarehe 7 Oktoba 2021 na Kituo hicho kinachotoa tuzo hizo za Nobel.
Tuzo hiyo inayotolewa na kituo hicho cha Sweden ina thamani ya corona milioni 10 za taifa hilo sawa na Sh bilioni 2.6.
Gurnah mwenye umri wa miaka 73 ni mwandishi wa riwaya 10, ikiwemo Paradise and Desertion.
Riwaya ya Paradise iliyochapishwa 1994, inaangazia hadithi ya mvulana aliyekulia nchini Tanzania katika karne ya 20 na kushinda tuzo ya Booker na kuanza kung’ara katika uandishi wa riwaya.
Yeye ni wa tano kwa jumla, baada ya Wole Soyinka wa Nigeria mwaka 1986, Naguib Mahfouz wa Misri, ambaye alishinda mwaka 1988; na washindi wa Afrika Kusini, Nadine Gordimer mwaka 1991 na John Maxwell Coetzee mwaka 2003.
ABDULRAZAK GURNAH NI NANI?
Licha ya kwamba si maarufu sana Tanzania na Zanzibar, lakini jina lake ni maarufu zaidi duniani.
Umaarufu huo haukutokana tu kwa kuwa Gurnah bali kutokana na umahiri wake katika lugha ya kiengereza na utunzi wa vitabu, Gurnah kwa hivi sasa ni Profesa wa lugha anafundisha katika chuo kikuu cha Kent kilichopo London Uengereza.
Gurnah alizaliwa Visiwani Zanzibar miaka 73 iliyopita, akiwa na umri wa miaka 17 alikimbia Zanzibar nna kuelekea Uengereza kwa lengo la kujiendeleza.
Aliondoka Zanzibar mwaka 1965 ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na mwaka mmoja baada ya Muungano wa Zanzibar na iliyokuwa Tanganyika.
Wakati huo fursa za kielimu zilikuwa haba kutokana na kuwepo kwa chuo kikuu kimoja tu maarufu Afrika Mashariki cha Makerere.
Baada ya kuondoka Tanzania alikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo ubaguzi nchini Uingereza. Akiwa hapo Uingereza licha ya changamoto hizo aliamua kujiendeleza hadi kuwa Profesa.
Umaarufu wake hautokani ukimbizi bali unatokana na uwezo wake na tuzo anazopata za utungaji wa vitabu bora ulimwenguni.
Akiwa nchini humo alioa mzungu ambaye anaendelea kuishi naye hadi sasa.
Gurnah baada ya safari yake ndefu ya ukimbizi kwa mara ya kwanza alirejea Zanzibar kutembea akiwa na umri wa miaka 32 mwaka 1980.
Leave a comment