Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateta na bosi TRC
Habari za Siasa

Rais Samia ateta na bosi TRC

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, tarehe 22 Mei 2021, amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa reli na maendeleo ya TRC. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Katika mazungumzo hayo, Kadogosa amemshukuru Rais Samia kwa Serikali ya awamu ya sita kuidhinisha kiasi cha Sh.372.34 bilioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha tano cha reli ya Mwanza – Isaka chenye urefu wa kilometa 341 kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railways).

Kadogosa ameeleza tangu Rais Samia aingie madarakani ujenzi wa reli katika vipande 2 unaendelea vizuri ambapo hadi mwezi uliopita kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (kilometa 300) kilikuwa kimefikia ya asilimia 91 na Morogoro – Makutupora (kilometa 422) kilikuwa kimefikia asilimia 60.02.

Amebainisha kuwa majaribo ya treni ya abiria yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa Agosti, 2021 kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro.

Kwa upande wake, Rais Samia amesema Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha ujenzi wa reli ya kati utakaounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi unakamilishwa ili kuzifikia nchi za Uganda, Burundi, Rwanda na DRC.

Amemtaka, Kadogosa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi vizuri ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutopora – Tabora, Tabora – Isaka na Kaliua – Mpanda – Kalema.

Rais Samia ameipongeza TRC chini ya Bw. Kadogosa pamoja na wote wanaoshiriki katika ujenzi wa reli kwa kazi nzuri wanayoifanya na ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya miradi hiyo.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, Ikulu ya Dar es Salaam, amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa reli na maendeleo ya TRC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!