Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa 421 kuchuana kuwania nafasi 10 ubunge viti maalum UVCCM
Habari za Siasa

421 kuchuana kuwania nafasi 10 ubunge viti maalum UVCCM

Spread the love

BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), leo Jumamosi tarehe 8 Agosti 2020 unafanya kura za maoni kwa wagombea wa ubunge na uwakilishi viti maalum, katika Uchaguzi Mkuu wa Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mkutano huo wa kura za maoni unafanyika katika Makao Makuu ya CCM Dodoma na kuongozwa na Kheri James, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.

Katika mchakato huo, vijana 421 wamejitosa katika kinyang’anyiro hicho cha kugombea nafasi 10 za Ubunge Viti Maalum kundi la vijana, Tanzania Bara na Zanzibar.

Wagombea 384 wanatoka Tanzania Bara wanawania viti sita, wakati 37 wanatokea Zanzibar wakiwania nafasi nne.

Kwa upande wa Uwakilishi viti maalum kundi la vijana, wamejitokeza vijana 40 wakiwania nafasi mbili.

Kura hizo za maoni zinafanyika baada ya mikitano ya UVCCM mikoa kupiga kura za maoni za kupendekeza wagombea tarehe 30 Julai mwaka huu.

 

Akizungumza katika mkutano huo, Pereira Silima, aliwataka wapiga kura hao kuendesha mchakato huo kwa uwazi na haki, ili kupata wagombea bora.

Naye, James amesema, matokeo ya mchakato huo si mwisho wa mchujo kwa kuwa vikao vitakavyofuata ndio vitaamua wagombea rasmi la umoja huo.

Amesema katika michakato ya kura za maoni za UVCCM katika mikoa uligubikwa na dosari mbalimbali, hivyo waliohusika na udanganyifu majina yao yatafyekwa.

 

“Ndugu zangu kazi mmeifanya mikoani, najua katika uchaguzi mkoa yako mambo mengi sio kwamba hatukuyaona wala kuyasikia, tumeona lakini leo tukamilishe kupiga kura kisha vikao vitakavyofuata vitaamu,” amesema James.

James amesema, wagombea waliodanganywa umri pamoja na kutumia rushwa ni miongoni mwa watakaokatwa majina yao katika vikao vya juu.

Amesema, kwa mujibu wa Katiba na Sheria, mbunge viti maalum kundi la vijana anatakiwa asizidi umri wa miaka 35 na asipungue miaka 21.

 

Kinachoendelea sasa ni wagombea hao mmoja mmoja kujinadi mbele ya wajumbe wa mkutano huo, kasha upigaji kura utafuatia.

Kesho Jumapili tarehe 9 Agosti 2020,Baraza Kuu la Wazazi litapiga kura za maoni kwa wagombea ubunge na uwakilishi viti maalum kundi la wazazi.

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), nao umeshafanya kura za maoni kupendekeza wagombea ubunge viti maalum kundi la wanawake.

 

CCM kilifungua zoezi la kutafuta wagombea wake katika uchaguzi huo tarehe 14 Julai mwaka huu, ambapo watia nia katika nafasi mbalimbali walianza kuchukua siku hiyo, na kisha kurejesha fomu hizo tarehe 17 Julai 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!