May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

40 Magufuli, Pengo ampa zawadi Mama Janeth

Spread the love

 

JOHN Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania, leo Jumanne, tarehe 27 Aprili 2021, amefikisha siku 40, tangu alipofariki dunia 17 Machi 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayati Magufuli, alifikwa na mauti saa 12 jioni ya siku hiyo, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Leo Jumanne, Mama Janeth Magufuli, Mjane wa Hayati Magufuli, akiwa ameongozana na Mary Majaliwa, Mkwe wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, wameshiriki Misa Takatifu ya kumwombea Hayati Magufuli, katika Kanisa la St Peters lililopo Osterbay.

Kanisa hilo, ndilo alikuwa akipenda kusali Hayati Magufuli, enzi za uhai wake tangu akiwa waziri n ahata Rais.

Pia, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, amemtembea nyumbani, Janeth Magufuli na kumkabidhi zawadi ya sananu ndogo ya Bikira Maria.

error: Content is protected !!