Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Michezo 40 kuingia kambini kuivaa Senegal
Michezo

40 kuingia kambini kuivaa Senegal

Spread the love

JUMLA ya wachezaji 40 wa kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite Queen kinatarajia kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya Senegal. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikosi hiko kinatarajia kuingia kambini tarehe 22 Septemba, 2020 hadi 5 Oktoba, huku kikiwa na wachezaji wanaotoka kwenye klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake.

Timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha Bakari Shime imefanikiwa kufika hatua hii mara baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Uganda kwa mabao 4-2 katika mchezo uliofanyika 1 Februari 2020 kwenye Uwanja wa Star Times mjini Kampala.

Senegal itacheza na Tanzania mara baada ya kufanikiwa kuitoa timu ya Taifa ya Sierra Leone kwenye hatua ya awali.

Michuanio hiyo inatarajia kufanyika nchini Costa Rica kuanzia 20 Januari, 2021 hadi 6 Februari 2021.

Majina kamaili ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi hiko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo Uingereza, Uholanzi zote kukupa pesa

Spread the love Siku ya leo EURO 2024 kupigwa katika viwanja mbalimbali,...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

error: Content is protected !!