LICHA ya Dk. John Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM na Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chadema kutawala siasa ngazi ya urais, Marekani imeeleza kutounga mkono mgombea wala chama chochote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Na kwamba, inaunga mkono kwa karibu mchakato wa demokrasia unavyoweza kushika hatamu kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.
Kwenye taarifa yake iliyotolewa tarehe 1 Oktoba 2020 kupitia ubalozi wake nchini hapa, Marekani imeeleza inaunga mkono haki na uhuru kabla, wakati na baada ya uchaguzi huo.
Taarifa hiyo imeeleza, Marekani na mataifa mengine wanafuatilia kwa karibu matendo ya watu wanaoingilia na kuvuruga mchakato wa kidemokrasia au kuchochea vurugu dhidi ya raia kabla, wakati au baada ya uchaguzi.
Taifa hilo limeeleza, linaunga mkono wito uliotolewa na wagombea wakuu kwa kuwapo mchakato wa uchaguzi wa amani na wenye uwazi.
“Tunatoa wito kwao na kwa wafuasi wao kuchukua hatua kutanzua hali ya uhasama inayojengeka na kuepuka matamshi ya kichochezi,” imeeza taarifa hiyo na kuongeza:
“Hatutasita kufikiria kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaobainika kuhusika katika vurugu na machafuko yanayohusiana na uchaguzi au kukwaza mchakato wa kidemokrasia.”
taarifa hiyo imefafanua kwamba, uendeshaji wa uchaguzi mwingine nchini utakuwa na matokeo muhimu si kwa Tanzania yenyewe pekee, bali pia kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Pia taarifa hiyo imeeleza, historia ya Tanzania ya kuendesha chaguzi zinazohusisha vyama vingi, inarudi nyuma hadi miaka 25 iliyopita na kuifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa Afrika.
I don’t have a website
Libepaul456@gmail.com