LAZARO Mamabosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Saalam amesema upigaji wa debe ni marufuku katika vituo vya daladala. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).
Mambosasa ameyasema hayo, leo tarehe 22 Novemba 2019, alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari juu ya uwepo wa wapiga debe katika vituo vya daladala licha kupigwa marufuku muda mrefu.
“Upigaji wa debe ni katazo la watu ambao wanataka kujipatia kipato bila kufanya kazi na hiyo inaingia pia kwenye uzululaji, Rais alipokuwa Morogoro ulisikia kuna mtu anajitambulisha mimi ni mpiga debe?
“Ni marufuku lakini kondakta na ajenti wanaruhusiwa kwa kuwa wanatosha kumfanya abiria akapokelewa na kupata huduma na maandalizi ya kusafiri,” amesema.
Amesema si wapiga debe tu ndio wanaendelea kuwepo pamoja na katazo ambalo limeshawahi kutolewa dhidi yao lakini hata wezi pia wanachukuliwa hatua za kisheria kila siku na hawaishi.
“Si unasema wapiga debe bado wapo, wezi wamekwisha? (akihoji), hapa wote tuna imani na tunaabudu kwenye dini tofauti ukienda msikitini utakuta sheikh anaendelea kukemea kuiba na kuzini na kutamani mali ya mtu mwingine, ukienda kanisani utayakuta hayo hayo, amri 10 za Mungu lakini humo humo kanisani acha simu yako nenda katoe sadaka halafu urudi ukiikuta ni habari nyingine,” amesema.
Amesema watu wajifunze namna ya kutii sheria bila kusubiri kushurutishwa na pia kila mmoja afanye kazi kupata mkate ulio halali.
Leave a comment