Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa 29 wauawa operesheni ya kumkamata mtoto wa El Chapo
Kimataifa

29 wauawa operesheni ya kumkamata mtoto wa El Chapo

Spread the love

 

TAKRIBANI watu 29 nchini Mexico wameuawa wakati wa operesheni ya umwagaji damu ya kumkamata mtoto wa kinara wa biashara haramu ya dawa za kulevya nchini – Joaquín Guzman maarufu kama El Chapo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Ovidio Guzmán-López (32), anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la zamani la baba yake linalojishughulisha na dawa za kukevya alikamatwa huko Culiacán na kusafirishwa hadi Mexico City juzi tarehe 5 Janruari, 2023.

Aidha, wakati na baada ya kukamatwa kwake askari 10 na washukiwa 19 waliuawa.

Wanachama wa genge lake wenye hasira waliweka vizuizi barabarani, wakachoma moto makumi ya magari na kushambulia ndege katika uwanja wa ndege wa eneo hilo.

Ovidio Guzmán-López

Waziri wa Ulinzi Luis Cresencio Sandoval alisema wanajeshi wengine 35 walijeruhiwa na watu 21 wenye silaha walikamatwa.

Guzmán-López – anayeitwajina la utani “Panya” – alipakiwa kwenye helikopta na kusafirishwa hadi mji mkuu kabla ya kupelekwa katika gereza la shirikisho lenye ulinzi mkali.

Anatumiwa kwa kuongoza kundi la baba yake maarufu la Sinaloa – mojawapo ya magenge makubwa zaidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya duniani.

Baba yake, Joaquín Guzman “El Chapo” anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani baada ya kupatikana na hatia mwaka wa 2019 ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

error: Content is protected !!