Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Lukuvi aunda tume maalum kuchunguza maafisa 183 wa Ardhi
Habari Mchanganyiko

Lukuvi aunda tume maalum kuchunguza maafisa 183 wa Ardhi

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi 
Spread the love

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 30 kwa timu maalum iliyoundwa kuchunguza maafisa ardhi 183 waliosimamishwa kazi hivi karibuni baada ya kuhusika na tuhuma za kuwafutia madeni wamiliki wa ardhi wanaodaiwa na kusababishia serikali hasara. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza Jijini Dodoma amesema taarifa za uchunguzi wa awali za miezi sita ya mwaka wa Fedha 2018/19 zimeonyesha watumishi hao kuchezea mfumo wa ulipaji kodi ya ardhi ambapo timu hiyo sasa itachungua kuanzia kipindi cha mwaka 2016 hadi sasa.

Alisema  kuwa timu hiyo itakuwa na wataalamu mwa mifumo ya kielektroniki, vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo wahusika wote watafikishwa mahakamani.

Waziri Lukuvi  pia alisema kuwa wamiliki wote wa ardhi waliofutiwa na kupunguziwa  madeni yao ya kodi ya ardhi hawako salama kwani walikusudia kukwepa kodi kwa makusudi na madeni yao yapo palepale na watalipa na adhabu.

Pia Waziri Lukuvi amemuagiza Kamishna wa Ardhi pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara kuwashughulikia wamiliki wa iliyokuwa Mbeya Hotel pamoja na Afisa Ardhi aliyempunguzia ukubwa wa kiwanja cha mita za mraba 20,234 na kuingiza kwenye mfumo mita za mraba 502.

“Kati ya kazi ambazo wizara ya Ardhi inafanya ni kusaidia serikali kukusanya mapato ya serikali pamoja na kusimamia chanzo kikuu cha mapato ya serikali ambayo ni kodi ya pango la ardhi,” alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema uhakiki huo wa miezi sita umebaini kuna watu walitakiwa kulipa kiwango fulani cha kodi ya pango lakini kiwango kilichoingia hazina ni kidogo ukilinganisha na kiwango kilichofutwa katika mfumo wa malipo ikionesha kiwango hicho kimelipwa.

Pia ameeleza kuwa kutokana na matokeo ya uhakiki huo Wizara kupitia kwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo wanaunda timu ambayo itayokuwa chini ya TAKUKURU na vyombo vingine vya usalama kuchunguza jambo hilo na makosa mengine yatakayoonekana katika uchunguzi huo.

Aidha Waziri Lukuvi amewatoa hofu wananchi kutokana na idadi kubwa ya maafisa ardhi waliosimamishwa amesema Shughuli za kiserikali katika Ofisi hizo zitaendelea kama kawaida.

Pia amewataka wananchi kutumia mfumo wa kielectroniki kulipia kodi ya pango ili kuepusha vitendo vya rushwa, pia ameongeza kuwa kwa wale wote ambao fedha za malipo ya pango zilifutwa bila malipo kuonekana kwenye mfumo na wale ambao malipo yao yameingia pungufu wote watalipa kiasi kilichobaki kukamilisha malipo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!