December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

27 waitwa kambini Stars, kuingia kambini Juni 5

Kim Poulsen Kocha wa Taifa Stars

Spread the love

 

KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen ameita kikosi cha wachezaji 27 kitakachoingia kambani tarehe 5 Juni, 2021 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi katika kujiweka sawa kuelekea mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia litakalofanyika Qatar mwakani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Kikosi hiko kimetangazwa hii leo jijini Dar es Salaam na Kim Poulsen kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Wakati wa kutangaza kikosi hiko Poulsen alisema kutakuwa na kambi za awamu mbili hii ya sasa mwezi wa sita na mwezi wa nane mara baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kukamilika lakini hakutakuwa na mabadiliko makubwa ya wachezaji.

“Kambi ya kwanza itakuwa mwezi Juni ambapo tutakaa kwa wiki mbili na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi ambao wamefuzu kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) na kambi nyingine itakuwa mwezi Agosti ambapo Ligi Kuu itakuwa imesha, ” alisema kocha huyo.

Aidha kocha huyo aliendelea kufunguka kuwa anahitaji timu yake kupata muda mrefu wa kujiandaa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji aliyowaita wanacheza kwenye Ligi ya ndani na kutoa pendekezo hilo kwa TFF.

“Kama tukiendelea kufanya vilevile tutaendelea kupata matokeo yale yale haya ndio niliwaambia TFF kwa hiyo tunatakiwa kubadilika, najua asilimia kubwa ya wachezaji niliowaita wanacheza kwenye ligi ya ndani, ” alisema Poulsen.

Mapendekezo ya kocha huyo kwa TFF hayakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kushauri kusimama kwa Ligi Kuu pale timu inapojiandaa na michuano ya kufuzu ili ipate muda wa maandalizi.

Mapendekezo yangu kwa TFF kama kocha wa Taifa stars tunapojiandaa na michezo ya kufuzu kuwepo na mapumziko kwa Ligi Kuu kwa Taifa Stars kupata muda wa wiki mbili au tatu kujiandaa na kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki,” alisisitiza Poulsen.

Kikosi kamili cha Taifa Stars ambacho kitaingia kambini tazama hapa chini.

error: Content is protected !!