Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Binti aondolewa kizazi kwa siri, madaktari washindwa kujieleza
Habari Mchanganyiko

Binti aondolewa kizazi kwa siri, madaktari washindwa kujieleza

Waziri wa Nchi Ofisi a Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Ummy Mwalimu
Spread the love

RAHAEL Alaay (25) ameiomba serikali kupitia Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuingilia kati mgogoro wake na Hospitali ya Wilaya ya Mbulu baada ya kuondodelewa kizazi kwa siri. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Raheli akizungumza na MwanaHALISI ONLINE leo tarehe 14 Machi 2019 amesema, tarehe 4 Aprili 2012 alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya uzazi lakini alitolewa kizazi bila ridhaa yake na hakuelezwa nia ya kuondolea kizazi chake.

Amesema kuwa, alifika hospitalini hapo saa nne asubuhi, alikaa wodi ya akina mama wajawazito mpaka saa saba mchana siku ya kesho yake.

Na kuwa, baada ya kukaa kwa siku hizo, manesi wawili walimpima na kumweleza kuwa, hawasikii mapigo ya moyo ya mtoto na kumueleza anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura.

Amesema kuwa, alifanyiwa upasuaji na Dk. Simon Slegray ambaye alimwondolea kizazi bila kumshirikisha yeye au familia yake lakini pia kutoa sababu.

“Nimefanyiwa upasuaji wa uzazi na kimsingi mtoto alitoka salama na anaendelea vizuri, ila mimi afya yangu imekuwa ikidhoofu mara kwa mara kutokana kuwa na maumivu makali tumboni.

“Nimetumia gharama kubwa kutafuta matibabu bila kujua, sikujua nasumbuliwa na nini nimeenda hospitali mbalimbali hadi nilipofanyiwa upasuaji lakini sikupata jibu la moja kwa moja.

“Baada ya kuangaika sana niliweza kwenda katika hospitali ya Babati Roman Catholic ambapo nilipimwa na kuambiwa kuwa, nina uvimbe tumboni ambao ulisababishwa na kuondolewa kwa kizazi,” amesema Raheli huku akitokwa na machozi.

Ameeleza kuwa, alianza kufuatilia ili ajue ni kwanini aliondolewa kizazi bila ridhaa yake wala kutojulishwa mtu yoyote wa karibu naye lakini hakupata majibu.

Amesema kuwa, amepeleka malalamiko hayo katika Hospitali ya Mbulu, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya lakini hakuna majibu yoyote ambayo yanaonesha kama kuna msaasa.

Aidha amesema, baada ya kugonga mwamba kila kona aliandika barua ya malalamiko na kuyaelekeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto ambayo aliiandika 26 Januari 2016.

“Baada ya barua hiyo, nilipokea barua kutoka kwa Msajili Baraza la Madaktari Tanzania yenye kumbukumbu Na.A.209/296/071 ya 10 Februari 2016 ambayo inaeleza kuwa, baraza hilo litafanyia utafanya utafiti kwa daktari aliyehusika na tukio hilo.

“Jambo linaloniumiza mimi ni kutopata majibu sahihi ya malalamiko yangu, ni ukweli kuwa siwezi kuzaa tena katika umri wangu wote, mbaya zaidi sina msaada wowote wa kimatibabu na nina maumivu makali lakini sina uwezo wa kujitibia kutokana na kuwa gharama yake ni kubwa.

“Ninaomba serikali iweze kuona uwezekano wa kunipatia matibabu ili kuweza kunusuru maisha yangu na ikumbukwe aliyenisababishia maumivu hayo ni mtumishi wa serikali,” amesema Raheli.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mbulu Mji, Christopher Nyalu amesema kuwa anatambua kesi hiyo lakini imeishaondoka kwa ngazi yake na ipo katika ngazi nyingine.

Alipotafutwa Msajili wa Baraza la Madaktari Tanzania DK. Palloty Luena amesema kuwa, malalamiko hayo ni ya muda mrefu na kueleza kuwa atafuatilia.

“Kesi hiyo itakuwa ni ya muda mrefu, nitafuatilia ili kujua ni kitu gani kinaendelea na nitarudi kwako ili kujua ni hatua gani zinaendelea,” amesema Dk. Luena.

Alipotafutwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alijibu kwa njia ya Whatsp kuwa, yupo nje ya nchi.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!