April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe, Ester Matiko wageuka kivutio bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Hai, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wote Chadema wamekuwa kuvutio katika ukumbi wa Pius Msekwa kwa kushangiliwa na wabunge baada ya kutambulishwa na Spika wa Bunge Job Ndugai. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Spika Ndugai aliwakaribisha wabunge hao muda mfupi kabla hajamkaribisha Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ili aweze kumkaribisha Waziri Wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ili aweze kuwasilisha mapendekezo ya serikali  ya mpango wa maendeleo wa taifa nay a kiwango cha ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambapo serikali inakusudia kutumia kiasi cha sh. Tilioni 33,105.4.

Ndugai alisema kuwa anatambua kuwepo kwa wabunge hao ambao kwa muda mrefu hawakuwepo na kwa lugha ya kibunge wanasema kuwa walikuwa Mtera.

Wakati akisema hayo wabunge wote walionekama kushangilia kwa furaha baada ya Mbowe na Matiko kutambulishwa.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu natambua uwepo wa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani … Makofi, Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mheshimiwa Ester Matiko…Makofi.

“Kwa Lugha ya kibunge tungesema walikwa Mtera waheshimiwa wote na watendaji wa serikali na watendaji wa Bunge ambao tupo pamoja nao ndugu waandishi wa habari mabini na mabwana Bwana Yesu asifiwe”alisema Ndugai.

Naye Waziri Mkuu alisema kuwa anatambua kuwepo kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kueleza kuwa anafurahishwa kuwa pamoja na wabunge wengine.

Matiko na Mbowe waliweza kukaa mahabusu ambao wamekaa huko takribani miezi mitatu kutokana na kukiuka mashariti ya dhamana.

Wakiwa katika ukumbi wa Piusi Msekwa wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao walionekana kuwafuata wabunge hao kwenye nafasi zao kwa lengo la kuwasalimia huku wabunge hao wakionekana kuwa na sura ya furaha.

error: Content is protected !!