Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais wa TFF achafua hali ya hewa, Chadema wamvaa
Habari za SiasaTangulizi

Rais wa TFF achafua hali ya hewa, Chadema wamvaa

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesikitishwa na kauli ya ukakasi iliyotolewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia juu na kile alichokiita U-Tundu Lissu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Karia aliitoa kauli hiyo leo katika Mkutano wa Mwaka wa TFF jijini Arusha, alipomfananisha Richard Wambura (aliyekuwa Makamo wa Rais wa TFF) na Tundu Lissu kuwa wanapaswa kushughulikiwa.

Soma taarifa kamili ya Chadema hapa chini.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).

TAARIFA KWA UMMA- KUHUSU KAULI YA KUFEDHEHESHA ILIYOTOLEWA NA RAIS WA TFF

Tumepokea kauli yenye ukakasi mkubwa iliyotolewa na Rais wa Chama cha Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ndugu Karia kuwa atawashughulikia wale wote ambao wataleta “U-Tundu Lissu” kwenye mpira.

Kauli hii inapaswa kutazamwa kwa umakini mkubwa kwani imebeba ujumbe mahususi kuwa watu aina ya Tundu Lissu wanastahili kushughulikiwa kwenye sekta zote.

Kwetu sisi kama Chama ni Kuwa watu aina ya ‘Tundu Lissu’ na wenye ‘U-Tundu Lissu’ ni wale wote ambao wenye mtazamo na uwezo wa kuhoji,  wanaotaka utawala wa sheria ufuatwe na wanaotaka sheria na Katiba ziheshimiwe na kuhakikisha kwamba kila mmoja anakuwa sawa mbele ya sheria na zaidi kila mwenye maoni na mawazo tofauti asikilizwe.

Sasa kauli ya Karia inatufanya tujiulize maswali mengi kama vile , inawezekana anawajua waliomshughulikia Tundu Lissu na ndio maana anataka kuwatumia kushughulikia ‘Tundu Lissu’ walioko kwenye mpira n.k.

Kutokana na kauli hii tunatafakari kuchukua hatua zifuatazo kama hataomba radhi;

1.Kusimamisha mahusiano na ushirikiano wowote na TFF ikiwemo kuwataka Wanachama wetu kutokushiriki matukio yote yanayoandaliwa na TFF.

2. Kususia bidhaa zote zenye nembo na au zinazotolewa na TFF zikiwemo jezi za timu za Taifa  na nyinginezo.

3. Kuchukua hatua dhidi ya Makampuni ambayo yataendelea kushirikiana na TFF ikiwemo Kususia bidhaa zao, kwani watakuwa wanaunga mkono taasisi inayoongozwa kwa ubaguzi wa kisiasa.

4. Kuwashawishi wadau wa mpira kokote kusitisha mahusiano na TFF Kwani inaendeshwa kisiasa na kibaguzi.

Tunamtaka Ndugu Karia aombe radhi hadharani na aeleze UMMA kauli yake ilimaanisha nini na kama anaona ni haki kwa Lissu kupigwa risasi na ndio njia sahihi ya kushughulikia changamoto za kwenye Mpira.

John Mrema

Mkurugenzi wa Itifaki,  Mawasiliano na Mambo ya Nje -CHADEMA

02 Februari, 2019

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!