August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

24 waitwa kambini Stars, kujiandaa dhidi ya Somalia

Spread the love

 

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania Kim Poulsen amita wachezaji 24, wa timu ya Taifa ya Tanzania watakaoingia kambini kwa ajili ya kujianda na michezo ya kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi hiko kitaingia kambini tarehe 15 Julai 2022, kwa ajili ya kaunza kampeni yake ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali hiyo zitakazofanyika Algeria.

michezo hiyo miwili yote itakuwa dhidi ya Somalia na yote itapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza utakuwa Julai 23 mwaka huu, ambapo Stars itahesabika ipo ugenini na mchezo wa marudiano utapigwa kwenye dimba hilohilo Julai 26 mwaka huu.

Fainali za michuano hiyo zinatarajia kutimua vumbi kuanzia Januari 8 mpaka Januari 31, 2023.

Na hiki ndio kikosi kamili.

error: Content is protected !!