March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Necta wafuta matokeo ya darasa la saba

Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendani wa NECTA

Spread the love

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limefuta matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wa mwaka 2018 katika shule zote za msingi wilayani Chemba mkoa wa Dodoma pamoja na nyingine nane, baada ya kubainika kukiuka kanuni za uendeshaji mitihani. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji NECTA, Dk. Charles Msonde amezitaja shule hizo ikiwemo Shule ya Msingi Hazina na New Hazina na Front Of Joy zilizoko jijini Dar es Salaam. Shule ya Msingi ya Alliance na New Alliance za jijini Mwanza, Shule ya Msingi Kondoa Intergrit na Farkwa zilizoko mkoani Dodoma.

Vile vile, Nacte imefuta vituo vya mtihani vya shule hizo baada ya kubainika kuvujisha mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wa mwaka 2018 uliofanyika terehe 5 na 6 Septemba mwaka huu.

“Katika mkutano wake maalumu uliofanyika leo baraza la mitihani ilipitia kwa kina taarifa hii ya uvujaji mitihani uliofanywa na maafisa wa mitihani. Necta imefuta matokeo ya kumaliza mtihani wa elimu ya msingi uliofanyika tarehe 5 na 6 Septemba 2018 kwa shule zote za msingi za halmashauri ya Chemba, Shule ya Hazina na New Hazina za Kinondoni, Front of Joy za Ubungo, na Alliance na New Alliance na Kisiwani za Mwanza jiji, na Kondoa Intergrit ya Kondoa mjini.

“Baraza pia katika maamuzi yake limeamua kuanzia sasa kufuta vituo vya mitihani vya shule za msingi hizo hadi hapo baraza litakapojiridhisha pasina shaka kwamba vituo ivyo vinauwezo wa kuzingatia sheria,” amesema na kuongeza Dk. Msonde.

Aidha, Dk. Msonde amesema Baraza limeamua shule zilizofutiwa matokeo kurejea tena mtihani huo wiki ijayo tarehe 8 na 9 Septemba 2018, na kutaja vituo vya muda ambavyo watahiniwa watavitumia katika kufanyia mtihani.

Dk. Msonde amevitaja vituo hivyo vya muda ikiwemo, kituo cha Shule ya Msingi Kakebe ambacho kitatumiwa na watahiniwa wa Shule ya Kisiwani kutoka jijini Mwanza, Shule ya Mahina ambayo itatumiwa na watahiniwa wa shule za Alliance na New Alliance, wakati watahiniwa wa shule ya Kondoa Intergrit wakipangiwa kufanyia mtihani katika shule ya Mbicha.

error: Content is protected !!