March 8, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bunge la Peru lamuondoa rais wake madarakani

Dina Boluarte

 

BUNGE la Peru limemuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo, Dina Boluarte kwa kura nyingi za wabunge, kufuatia hoja za kutokuwa na uwezo wa kudumu wa maadili katika kutekeleza majukumu yake. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Raisi huyo ameondolewa madarakani usiku wa tarehe 9 Oktoba 2025 na kutangazwa na spika wa bunge José Jerí na kusema anaweza kujitetea au kuakilishwa na wakili na kudai kuwa katika kikao hicho rais Boluarte hakufika licha ya kutakiwa kuhudhuria

Kutimuliwa kwa rais kumeidhinishwa, anaweza kujitetea au kuwakilishwa na wakili” ametangaza Spika wa Bunge José Jerí ametolewa madarakani kupitia kura zilizopigwa na wabunge 87 kati ya 122 walioshiriki katika kura hiyo, walilazimika kupiga kura kuunga mkono kuondolewa kwake.

Kabla ya kura hizo vyama vikuu vya kisiasa katika Bunge viliwasilisha hoja tano za kumtimua madarakani wakati wa mchana uchunguzi wa hoja nne kati hizo zilipitishwa kwa kura nyingi katika Bunge la nchi hiyo.

Ikumbuke kuwa rais Boluarte alipata nafasi hiyo kupitia kuondolewa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Pedro Castillo kutokana na jaribio la kutaka kuvunja bunge mwaka 2022 kipindi hicho rais Boluarte akiwa makamu wake.

About The Author

error: Content is protected !!