Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa 2022 Mwaka ulioitikisa China
Kimataifa

2022 Mwaka ulioitikisa China

Spread the love

MWAKA 2022 ulikuwa mwaka wenye changamoto kwa Serikali ya China hasa wakati inakabiliana na kudhibiti ugonjwa wa Uviko-19. Imeandikwa na chombo cha habari ANI News Services … (endelea).

China kupitia chama chake tawala cha Kikomunisti (CCP) kimeufundisha ulimwengu namna kilivyo bora kwenye kudhibiti idadi ya watu wake, lakini hakijakamilika katika kutawala watu.

Mwaka 2020 Serikali ya China ikiwa kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona ilijikita kwenye matumizi ya mbinu ya kuweka watu kwenye vizuizi.

Wananchi waliishiwa uvumilivu na kuchoshwa na hali hii pale ambapo vizuizi vilisababisha wakazi kadhaa katika jengo la Urumqi kufariki kwa kuungua moto kwenye jengo hilo wakiwa kwenye kizuizi.

Hali hii ilisababisha maandamano katika miji mbalimbali chini na kutoa taswara ya kuchokwa kwa serikali kutokana kushindwa kuwa na mbinu nyingine ya kupambana na corona na kusababishia wananchi maumivu.

Bado lawama zitaelekezwa kwa CCP na Serikali yake hasa kushindwa kuwekeza kwenye chanjo bora, kitengo cha wagonjwa mahututi akiba ya dawa na kampeni ya chanjo kwa wazee badala yake ikipiga kufuli na kuwaweka watu vizuizini.

Kampuni ya utabiri ya Akili ya Sayansi Airfinity,  inakadiria kuwa kesi zinaweza kufikia milioni 3.7 kwa siku mnamo Januari na milioni 4.2 mnamo Machi. Hivi sasa, labda kuna vifo zaidi ya 5,000 vya kila siku, wakati Beijing, imekuwa ikiripoti kwa uwongo wastani wa vifo saba tu kwa wiki.

Nchi zimezidi kuweka vikwazo vya usafiri au majaribio kwa wasafiri kutoka Uchina, huku hofu ya aina mpya za COVID ikiongezeka. CCP iliruhusu wasafiri kueneza coronavirus ulimwenguni mapema 2020, na inafanya vivyo hivyo sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!