August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

2017 mwisho mifuko ya plastiki

Spread the love

SERIKALI imesema kwamba ifikapo Januari Mosi mwaka 2017 utakuwa ni mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki nchini, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na January Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wakati akijibu swali la nyomgeza la Edward Mwalongo, Mbunge wa Njombe Mjini (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itapiga marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki ambayo inaonekana kuwa kero kwa uchafuzi wa mazingira.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua kama serikali haioni kwamba umefika wakati wa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Akijibu swali la nyomgeza Makamba amesema kwamba, ifikapo Januari Mosi mwaka 2017 utakuwa ni mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki kwani inaonekana kuwa kero kwa uchafuzi wa mazingira.

error: Content is protected !!