JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 68 kwa tuhuma za kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji katika Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 18 Agosti, 2018 na SACP Ulrich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
Kamanda Matei amesema watuhumiwa hao ambao wanaume wako 62 na wanawake 8, katika msako mkali uliofanywa na polisi tarehe 17 Agosti, 2018 katika Kijiji cha Ngole.
“Awali mnamo tarehe 14 Agosti mwaka huu kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Ngole, watuhumiwa hao kwa makusudi na bila uhalali waliharibu mabomba na vyanzo vya maji kwa kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya takribani Sh. 14 milioni, mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni michango ya baadhi ya wanakijiji na wafadhili,” amesema Kamanda Matei.
Kamanda Matei amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Leave a comment